Makabidhiano hayo yamefanyika katika ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mpimbwe mbele ya Wakuu wa Idara na Vitengo leo 14 /06 /2023.
Akibidhi ofisi amewashukuru Viongozi wote Wa Mkoa wa Katavi, Watumishi, na Wananchi wote wa Halmashauri ya Mpimbwe kwakutoa ushirikiano mzuri kwa kipindi chote cha miaka 3 aliyokuwepo katika Halmashauri hii ya Mpimbwe.
Pia amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuendelee kumuamini kufanyakazi ya kuwatumikia wananchi katika Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ambapo atakuwepo kuanzia hivi sasa.
Aidha amemkabidhi Bi. Shamimu Mwariko miongozo mbalimbali ya Halmashauri, Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM ,Watumishi wote, Wananchi wote , Madiwani ,Tarafa Mbili ya Mpimbwe, na Mamba, Mbunge Mmoja, Kata , vijiji , vitongoji na Taasisi zote.
Akipokea ofisi Bi . Shamimu Mwariko amesema anamshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Kumleta katika Mkoa wa Katavi na Halmashauri ya Mpimbwe ilikuweza kuendelea kuwatumikia Wananchi wa Tanzania.
Mwariko amesema ushirikiano Kujitoa nakufanya kazi kwa moyo hii itasaidia katika kuendeleza Taifa letu.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa