Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bw. Erasto N. Kiwale (Kulia) aliyesimama akimkabidhi Ofisi Mkurugenzi Mtendaji Mpya wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Michael Mashalla tayari kwa kuanza kazi. Aidha Mkurugenzi huyo Mpya ameomba kufanya kazi kwa ushirikiano katika kuwaletea maendeleo wana Mpimbwe kama serikali ilivyokusudia nae Mkurugenzi aliyehamishwa kwenda Manispaa ya Kigamboni amewashukuru Wakuu wa Idara na Vitengo kwa Jinsi walivyompa ushirikiano katika kipindi chote cha Uongozi wake Mpimbwe hadi alipopata uteuzi wa Kuhamishwa kituo cha kazi kwenda kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Kigamboni
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa