Wakichangia taarifa ya utekelezaji wa ujenzi barabara iliyowasilishwa na meneja wa TARURA Mhandisi Maneno Makorongo juu ya ukarabati wa barabara za halmashauri hiyo katika kikao cha baraza la madiwani kilicho fanyika tarehe 27/10/2022 katika ukumbi wa halmashauri hiyo madiwani wameelezea kusikitishwa kuona barabara zinashindwa kukamilika kwa wakati ikiwa madiwani hao wamefanya juhudi kubwa ya kuwahamasisha wananchi kushiriki ujenzi huo kikamilifu.
Awali, akitoa ufafanuzi katika kikao cha baraza la madiwani leo meneja wa TARURA Mhandisi Makorongo amesema tatizo la kuchelewa kukamilika kwa ujenzi wa miundombinu ya barabara hizo imesababishwa na changamoto ya uhaba wa wakandarasi jambo ambalo limepingwa na mwenyeketi wa Halmashauri ya Wilaya hiyo Mhe. Sailas Irumba.
"Nchi hii ina wakandarasi wengi tunataka wananchi wetu waweze kuneemeka na pesa anayoitoa Mhe. Rais kwenye TARURA" Amesema Mhe. Sailas Irumba Mwenyekiti wa halmashauri ya Mpimbwe.
Wakitoa ushauri kikaoni hapo, baadhi ya madiwani wamemshauri mhadisi kuwa afanye ukaguzi wa vifaa vya wakandarasi wake kabla ya vifaa hivyo kuanza kufanya kazi ili kuondoa usumbufu wa kukwama kwa zoezi la ujenzi kwa muda uliopangwa.
Mara baada ya mwenyekiti kutoa ufafanuzi wa kina juu ya changamoto wanazozipata wanachi katika maeneo ya miradi hiyo ya barabara, meneja wa TARURA Wilaya ya Mlele ameahidi kikaoni hapo kuwa atazingatia ushauri uliotolewa na waheshimiwa madiwani hao na kuufanyia kazi.
MWISHO.
*Imetolewa na.*Kitengo cha mawasiliano Serikalini.*Halmashauri ya Mpimbwe*
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa