Akizungumza na Wananchi wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo 2022/2023 uliofanyika kata ya Usevya Halmashuri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi, Mkuu wa Wilaya ya Mlele amekemea swala la wakulima kutoweka akiba ya chakula kwa kuuza mazao yote.
Mhe. Filbarto Sanga amesema kila Mkulima anapaswa kuweka akiba ya mazao yake yatakayo muwezesha kumfikisha katika msimu mwingine wa kilimo ilikuweza kuepukana na maswala ya njaa katika familia , kutokana na kuwepo kwa mabadiliko ya tabia nchi yanayoweza kusababisha mvua kuwa chache , na kutopata mazao kwa wingi .
Amesema baadhi ya wakulima wamekuwa wakipata tamaa ya kuuza mazao yao yote waliolima na kuanza kulalamika njaa na kuhitaji serikali iwape msaada swala ambalo kwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe halitakiwi kusikika kwa kuwa Ardhi ya Mpimbwe ina rutuba na inafaa kwa kilimo.
“Niaibu kwetu kusikia familia inasema sisi tunanjaa wakati tunajua mwenye familia ile nimkulima alilima na chakula kilikuwepo kwenye hilo ajiandae kupelekwa mahakamani , haiwezekani umeshindwa kusimamia familia yakwako wewe mwenyewe shamba unalo umelima umevuna , umeingia tamaa ya kuuza bila utaratibu nabado wataka Sereikali ikusaidie haiwezekani” alisema
Mhe.Sanga amewashauri wakulima kutumia mbegu za kisasa ambazo zitachukua muda mfupi shambani na zitakazoweza kutoa mavuno mengi Zaidi.
Aidha amesema swala la wakulima kulima na kukata Miti katika maeneo ya vyanzo vya maji vimekuwa vikwazo vikubwa ambavyo vinasababisha kukosekana kwa maji katika meneo mbali mbali .
Awali akizungumza Mkurungenzi Mtendaji Halmashauri ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla amesema Halmashauri hiyo ni Halmashauri amabayo inategemea mapato kutokana na uzalishaji katika kilimo hivyo amewataka wananchi kulima mazao ambayo yatawaletea tija Zaidi katika familia na katika Serikali .
Mwisho.
Imetolewena;
Kitengo cha mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa