Naibu waziri wa Ardhi nyumba na maendeleo ya Makazi na Mbunge wa Jimbo la Kavuu Mhe. Geofrey Pinda ameshuhudia ugawaji wa Magari mawili yatakayosaidia kurahisisha utoaji wa huduma za Afya katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe leo tarehe 03/02/2024.
Zoezi hilo la ugawaji wa magari mawili limefanyika katika Kituo cha Afya Usevya ambapo viongozi mbalimbali wa Halmashauri pamoja na wananchi walihudhulia.
Akitoa taarifa, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe Dr. Martin Lohay amesema magari hayo yatasaidia kurahisisha huduma za Afya hasa mama wajawazito na kuepusha vifo vya mama na watoto wachanga kwani awali lilikuwa gari moja tu lililotumika kubeba wagonjwa halmashauri nzima.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Shamim Mwariko ameishukuru Serikali inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha huduma katika jamii na kutoa fedha za kuendeleza miradi mbalimbali.
Pia amemshukuru Naibu Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi na Mbuge wa jimbo la kavuu kwa kuendelea kuongeza jitihada kubwa serikalini kwa ajili ya kutetea kuongeza miradi. Hivyo, Mkurugenzi ameahidi kuendelea kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili iendelee kuleta manufaa kwa wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa