Na Odetha salum.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe yaibuka kinara baada yakuchukua nafasi ya Kwanza kumaliza Ujenzi Wa Madarasa yatokanayo na Fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mh.Samia Suluhu Hassan.
Kati ya Halmashari Tano ambazo ni Halmshauri ya Nsimbo, Halmashauri ya Mlele, Halmashauri ya Tanganyika, Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda, na Halmashauri ya Mpimbwe, ambazo zilitakiwa kufikia tarehe 9 Disemba 2021 ziwe zimekamilsha Vyumba vya Madarasa kutokana na taratibu zilizopangwa kimkoa.
Akizungumza mgeni rasmi katika makabidhiano ya Miradi ya Ujenzi wa Madarasa,Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua Mrindoko amesema Kimkoa ilipangwa kufikia tarehe 9 Disemba 2021 madarasa yote yawe yamekamilika lakini mpaka sasa Halmashauri ya Mpimbwe ndiyo Pekee iliyoweza kukamilisha Kwa wakati jambo linaloonesha ushikamano na hali yali yauchapaji kazi katika Halmashauri ya Mpimbwe
Aidha amezitaka Halmashauri zote kufika tarehe 15 Disemba 2021 ziwezimekamilisha Ujenzi wa Madarasa pamoja na Madawati na viti na meza ilikuweza kukabidhi Kitaifa.
Sanjari na hayo amewataka wananchi wote kulima Mazao yanayo stahimili ukame na kutumia Mbegu zinazo komaa mapema kutokana na Mkoa Wetu kupata Mvua za wastani na zilizo chini ya wastani.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa