Kamati ya imesisitiza ujenzi wa vyumba 23 vya madarasa uzingatie viwango stahiki vilivyoelekezwa na serikali na ukamilike December07,2022
Kamati ya ufuatiliaji wa miradi ya maendeleo mkoa wa Katavi imefanikiwa kukagua ujenzi wa vyumba vya madarasa 23 katika Halmashauriya Mpimbwe wilaya ya Mlele leo tarehe10.11.2022.
Kamati hiyo imekuja ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ikiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo teule Ndg.Ngeshere Serubu kutoka mkoa wa Katavi,Ndg.Philipo Charles katibu wa kamati hiyo ambaye ni mhandisi kutoka Mkoa wa Katavi Pamoja na wajumbe walio ambatana nao ambao ni Afisa Mipango Mkoa Wilson Kenedy,Siza Nassoro kutoka ofisi ya manunuzi Mkoa ambapo wameelezea kuwa miradi hiyo inaendelea vizuri na wamesisitiza viongozi ndani ya wilaya hiyo kuendelea kuisimamia vizuri ili ifikapo 07.12.2022 iwe imekamilika.
Kamati hiyo imefanikiwa kutembelea MIradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa 13 shule ya Sekondari Majimoto,ujenzi wa vyumba vya madarasa 4 shule ya sekondari Mamba,vyumba vya Madarasa 2 shule ya sekondari Usevya,ujenzi wa darasa1 shule ya sekondari kasansa na ujenzi wa vyumba 3 vya madarasa shule ya sekondari Chamalendi.
Katibu wa kamati hiyo ambaye ni Mhandisi Philipo Charles kutoka Mkoani ameagiza ujenzi huo usimamiwe kikamilifu na watendaji ndani ya Halmashauri hiyo ikiwa ni Pamoja na kusimamia kila hatua ya ujenzi huo ili kuepusha matumizi mabaya ya fedha hizo.
Ikumbukwe kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ilipokea kiasi cha shilingi milioni 460,000,000 kutoka Serikali kuu kwaajiliya ujenzi wa vyumba vya madarasa 23 katika Halmashauri hiyo.
Mhandisi Emmanuel Mugenyi ameelezea kuwa maelekezo ya kamati hiyo wameyapokea na kuahidi kuyasimamia kikamilifu.
"Tunashukuru sana kwa kututembelea kamati hii na maelekezo yote tumeyapokea na tunaahidi kuyafanyia kazi kikamilifu,miradi yote itaka milika mapema kabla ya tarehe ya mwisho, Halmashauri ya Mpimbwe tumejipanga kikamilifu kuhakikisha kila shilingi inatumika kama ilivyoelekezwa na viongozi wa wizara ili kukidhi malengo ya Serika li kuhakikisha ujenzi huu unakwenda kuwasaidia wananchi na wanafunzi chini ya uongozi madhubuti wa awamu ya sita wa Mhe Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania." Amesema Mhandisi Mugenyi.
Imetolewana. Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa