Naibu Waziri wa kilimo Anthony Mavunde amefanya ziara katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa Katavi , ambapo ametembelea Skimu ya umwagiliaji katika kijiji cha kilida kata ya Mamba na kugawa matrekta ya Mkono yaani Powertillers kwa wakulima waliokopeshwa na Kampuni ya ZANA BORA kupitia Benk ya NMB.
Akisoma Taarifa Ndugu George Magile Mkuu wa Idara ya kilimo amesema Katika kuhakikisha Wakulima wanapata huduma bora Halmashauri imeweka mkakati wa kuboresha huduma za ugani kwa kuhamasisha wakulima wajiunge katika vikundi iliwaweze kufikiwa kwa urahisi na mpaka sasa vikundi 59 vimeanzishwa katika kata mbalimbali za Halmashauri yaWilaya ya Mpimbwe.
Jumla ya Wakulima 2134 wamepata mafunzo ya uhifadhi nafaka salama na wa wakulima 1937 wamepata mafunzo ya kilimo bora cha mbongamboga na Matunda .
Aidha wakulima wamepata elimu juu ya matumizi sahihi na salama ya viuatilifu na matumizi sahihi ya mbolea na mbegu bora, kuboreshwa miundombinu ya Kilimo kwa kukarabati na kujenga mifereji ya umwagiliaji kwa lengo la kupunguza upotevu wa maji, jumla ya Km3.5 za Mifereji zimeboreshwa kienyeji pia jumla ya km 59 za barabara zimekarabatiwa ili kurahisisha usafirishaji wa mazao ya wakulima.
Ndg. Magile amesema katika Halmashauri ya Mpimbwe Maghala ya kuhifadhia mazao 10 yaliyojengwa na Serikali yanatumika na Maghala 147 ya watu binafsi yanatumika kuhifadhia mazao ya Wakulima.
Aidha Wakulima katika msimu huu wa kilimo toka vyama vya msingi AMCOS wameweza kukopeshwa fedha na pembejeo za kilimo zenye jumla ya Tsh 2,074,480,000
Jumla ya wakulima 53 wamepata Trekta za mkono yani powertillers zenye thamani ya TSh. 683,700,000
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kavuu Mh. Geofrey Pinda ameishukuru kampuni ya ZANA BORA kwa kushirikana na Benki ya NMB kwa kutoa zana hizo zitakazo saidia wakulima katika kuzalisha mazao.
Naibu waziri wa kilimo Mh.Anthony Mavunde amesema “bonde Hili ni muhimu kwa nchi yetu ya Tanzania hasa katika uzalishaji wa mazao mnaoufanya hapa, ndio maana sisi kama Wizara Tunaliangalia bonde hili kwa jicho la tofauti tukiweka nguvu hapa tutaisaidia Tanzania na siyo Mkoa wa Katavi peke yake”
Mh .Mavunde amesema katika malengo ambayo Serikali imejiwekea nikuwa na uzalishaji mkubwa wa Mazao hasa ya nafaka kufikia ziada ya kuuza Nje ya nchi, ili kuweza kufikia malengo hayo tusilime kilimo cha kutengemea mvua peke yake badala yake tujikite katika skimu za umwagiliaji.
Aidha Mh. Mavunde amesisitiza kuendelea kutumia Teknolojia za kisasa ili kuweza kuacha kulima kwa kutumia jembe la mkono na badala yake kutumia Trekta.
Na Odetha Salum
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa