Sikukuu hii huadhimishwa kila ifikapo tarehe 15 Mwezi 10 kila mwaka ambapo yamefanyika katika Kijiji cha Kabunde Kata ya Mamba Halmashauri ya Mpimbwe.
Maadhimisho haya yenye Kauli mbiu inayosema WEZESHA WANAWAKE WANAOISHI KIJIJINI KWA UHAKIKA WA CHAKULA, LISHE NA UENDELEVU WA FAMILIA yanalengo la kutambua jitihada ya Mwanamke anaye ishi kijijini, kuongeza mwitikio wawanawake kushiriki katika Uchumi, upangaji na utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika maeneo yao, kujenga uelewa wa fursa za kiuwezeshaji wanawake katika uchumi na namna bora yakukabiliana na umaskini wa kipato na upatikanaji wa chakula katika kaya.
Akizungumza Mgeni rasmi katika Maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Majid Mwanga amesema Serikali imejitahidi katika kuboresha Miundombinu ambayo mhanga mkubwa ni Mwanamke anayeishi kijijini hivyo Serikali imeleta huduma mbalimbali vijijini ikiwemo huduma za Umeme, Maji , Barabara Vituo vya Afya na Zahanati pamoja na huduma nyingi zitakazo msaidia mwanamke anayeishi kijijini kujikwamua kiuchumi na kuleta ustawi katika Jamii.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Mwariko amesema Mwanamke ninguzo kubwa katika familia hivyo anapaswa kuhakikisha familia inakuwa na chakula chakutosha ilikuweza kuepusha njaa katika familia , uhifadhi mzuri wa Mazao yanayo patikana uwezekuzingatiwa ilikuweza kuepuka kuharibika kwa Mazao na kuhakikisha uwepo wa chakula bora.
Estar Sabato ni Afisa Lishe katika Halmashauri ya Mpimbwe naye amesema ili kuweza kupata watoto wenye afya njema na wenye akili lazima Mama mjamzito ahakikishe anapata chakula bora wakati wa ujauzito na pia ahakikishe anakwenda Kliniki mala tu anapogudua kuwa ni mjamzito.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa