Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.Philip Isdor Mpango amesema watumishi wa Umma wanapaswa kutumia majengo kwakutatua changamoto za wananchi kwakuzingatia sheria na taratibu za umma nasiyo kutumia kupokea rushwa na ufisadi.
Makamu wa Rais amesema hayo leo Tarehe 22. Julai 2022 wakati akizindua Jengo la Utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambalo limegharimu kiasi cha Shilingi Bilioni 2.9 amesema fedha zinazo tolewa na serikali zifanye kazi kwa uadilifu mkubwa.amesema imefika wakati wa watumishi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na badala yake wanapaswa kufaya kazi kwa upendo mkubwa.
Aidha ameagiza wizara ya maji kuhakisha suala la changamoto la maji Usevya linakamilika kufikia Novemba mwaka huu kwa kutumia mradi unao toka majimoto mpaka usevya.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Kavuu ambaye pia ni Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Mh. Geofrey Pinda amiomba serikali kuanzisha wilaya ya kipolisi katika Halmashauri ya Mpimbwe Pamoja na uwepo wa Gereza ili Wananchi wapate huduma kwa urahisi
Naye Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi. Mwanamvua mrindoko ameishukuru serikali kwa kutoa fedha nyingi kwa ajiliya ujenzi wa majengo saba ya utawala katika Mkoa wa Katavi yatakayo saidiwa kutoa huduma na kufanyakazi kwa Watumishi.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa