Wakizungumza baadhi ya wafanyabishara katika kikao kilicho fanyika katika ukumbi wa shule ya Sekondari Usevya, wafanyabiashara wamesema wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ya kutozwa ushuru mkubwa ukilinganishwa na mapato wanayoyapata hali inayopelekea wafanyabishara wengine kuhamia maeneo mengine ambayo yanatozo ndogo ya Ushuru, jambo ambalo halimwathiri mfanyabiashara pekeyake bali, linamwaathiri mkulima pia, hali itakayo pelekea kushuka kwa mapato ya Halmashauri.
Pia wamesema kuna mashine iliyopo Mwamapuli ambayo inaweza kufanya Mpibwe kutoa mchele Bora utakao weza kuuzwa kimataifa, Mashine hii imekuwepo na haifanyi kazi, hivyo wanaomba utaratibu stahiki ufatwe ili ianze kufanyakazi, hii itatoa fursa kwa wafanyabishara kuweza kutanua wigo wa fursa zingine, kuepukana na udhalishaji wa mchele kwa kiwango Cha chini.
Aidha; wamesema kuwepo kwa changamoto mbalimbali ikiwemo maji, umeme kukatika mala kwa mala na miundombinu ya barabara kuwa mibovu kunakwamisha shughuli za kimaendeleo.
Kwa upande wake mkurungezi wa halmashuri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkurungenzi Catherini Mashalla akijibu baadhi ya maswali ya wafanyabishara amesema anahidi kurekebisha tozo za ushuru, ambapo kwa Sasa gharama ya gunia moja ni 3,500 ikiwa ni maazimio ya kikao cha wadau kilicho fanyika katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Katavi hivyo amesikia kilio cha wafanyabiashara, lakini pia amesema kutokana na maswala ya maji imepangwa maji kufikia kila kata kutoka katika kata ya Mamba. Pia mashine iliyopo mwamapuli ni mashine ya kisasa lakini inatumia mafuta hivyo iko katika mchakato wa kuanza kutumia umeme ili iweze kufanya kazi vizuri na kwa ufanisi mzuri.
Mh Catherini ameongezea kuwa ipo mikopo inatolewa kwa makundi matatu; Wanawake, Vijana, na watu wenye Ulemavu na kuwashauri kuweza kuanzisha kiwanda cha kutengeneza vifungashio kwa ajiri ya kufungashia bidhaa na vyenye nembo ya Mpimwe ilikuweza kutangaza Wilaya
Sanjali na hayo amesema changamoto iliyopo katika kituo cha Afya nikutokana na kituo kuelemewa kwa kuhudumia watu wa kata zote kama Rufaa ya mpimbwe hivyo kusubiria mradi wa Hospitari ya Tupindo kukamilika ilikuweza kuwa kama Rufaa.
Hivyo ameshauri wafanayabishara kuweza kuanzisha viwanda kwa ajiri ya kuchakata nafaka kabla ya barabara zote kukamilika ili watakapokuja wafanyabiashara wakubwa wakute tayari viwanda vipo na vina fanya kazi.
Naye Naibu waziri wa sheria na katiba MH: Geofrey Pinda Akijibu maswali ya Wafanyabiashara amesema wapo watu wanao omba kazi kwa kumpatia Fedha mwajiri ili aweze kumpatia kazi sasa ikiwa mtu atampatia mtu Rushwa akifahamika lazima aondolewe kazini.
Pinda amesema mchele unaotoka mpimbwe ni mchele ambao unaradha hivyo amewataka wafanyabiashara kuutangaza kwa kuweka nembo zenye kuonesha wapi unatoka kwa sababu ni mali ya Mpimbwe wa nasiyo vinginevyo.
Aidha amesema waziri wa Tamisemi Ummy mwalimu ameacha fedha nyingi kwa ajili ya miradi mbalimbali inayoendelea.
Hata hivyo amewataka wakulima kulima mahindi kwa ajili ya chakula Zaidi wakulima wajikite katika mazao ya biashara kama vile Alizeti, Kalanga na Ufuta ilikuweza kupata wanunuzi wa halaka na kujipatia kipato cha halaka kutokana na uhaba wa mafuta uliopo Nchini.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa