Mh.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa rasmi leo amezindua kituo cha redio katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ijulikanayo kwa jina la Mpimbwe Fm redio 88.5 Mhz. Katika uzinduzi huo Waziri Mkuu amewataka wakuu wa idara kutatua matatizo ya wananchi kupitia redio hiyo.
Pia ameipongeza wizara ya Teknolojia ya Habari na mawasiliano kwa kushirikiana na shirika la USCAF Kwa utekelezaji wa kituo hiki cha redio.
Waziri Mkuu amempongeza Mbunge wa Jimbo la kavuu Mh Geofrey Pinda kwa kuendelea kutekeleza Miradi mbalimbali inayofanywa na serikali ya Jamhuri ya Mungano wa Tanzania ikiongozwa na Daktari Samia Suluhu Hassan.
Kupitia utekelezaji huo Pia Mh Kassim Majaliwa amewasihi wananchi kutumia redio hiyo kutangaza biashara zao ikiwemo mazao yanayotokana na kilimo.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa