Mh.Geofrey Pinda Naibu Waziri wa Sheria na Katiba Pichani ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Kavuu akizungumza na Wah.Madiwani na Watumishi wa Halmashauri ya Mpimbwe leo tarehe 31 Dec. 2020.
Aidha Mh.Pinda aliwataka Wah.Madiwani kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na wafanyakazi wengine na kuepuka kutengeneza migogoro isiyo ya lazima ili kuharakisha maendeleo kwa Wananchi kama ilivyo azma ya Mh.Rais Dr.Joseph Pombe Magufuli ambaye kila siku anasisitiza kuwa uongozi ni kutumika na siyo kutumikiwa.
Sambamba na hilo Mh.Naibu Waziri alitoa takribani kiasi cha Tsh. mil.40 fedha za mfuko wa Jimbo katika ukamilishaji wa miradi mbalimbali ya shule za msingi na Sekondari, Zahanati na Vituo vya Afya na kuwataka watendaji na Wah. Madiwani wakakamilishe miradi hiyo haraka iwezekanavyo ili ikatoe huduma kwa wananchi.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa