Mh. Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko, ametembelea mabanda ya maonyesho ya Nanenane yaliyopo katika viwanja vya Mwakangale Mkoani Mbeya.
Akiwa anaongea na wananchi pamoja na wajasiliamali wa mkoa wa katavi, amewapongeza wajasiliamali hao kwa ubinifu wanaendelea kuufanya katika kudhalisha bidhaa zao pamoja na kushiriki maonyesho ya Nanenane.
Pia amesisitiza kuboresha vifungashio vya bidhaa ili viwe na ubora unaitakiwa. " Wakurugenzi andaeni utaraibu mzuri wa upatìkanaji wa vifungashio vinavyotambulisha taasisi zenu" Alisema.
Na amesisitiza kutenga maeneo ya uwekezaji kwa ajili ya kilimo na mifugo hasa kwa makundi ya vijana na wanawake pamoja na wanawake ikiwa ni pamoja na kutenga fedha za mikopo kwa makundi hayo.
Mh. Mrindoko ameitaka jamii ya wanakatavi kutumia fursa zinazotelewa na Serikali ya awamu ya sita ikiwemo upatikanaji wa pembejeo za kutosha, hivyo amewataka wananchi kuendelea kuzalisha kwa wingi. " Serikali imeandaa mazingira mazuri ya uuzaji wa bidhaa za kilimo na mifungo hivyo wananchi tuendelee kuzalisha"
Kisha amewataka wakurugenzi kuwa na utaratibu wa kuwatembelea wajasiliamali kwenye maeneo yao ili kujua çhangamoto wanazozipitia sambamba na kuwawezesha.
Katika hotuba yake amegusia kufanyika utambuzi wa viwanda vidogo vyote vilivyopo Mkoani Katavi ikiwa ni pamoja na kuwaunganisha wajasiliamali hao na VETA ili kuongeza ujuzi.
Baada ya ukaguzi huo, Mh Mrindoko alipata fursa ya kuupokea ugeni wa Mh Tulia Akson Spika wa Bunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
MWISHO.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa