Akizungumza leo mbunge wa jimbo la kavuu Geofrey Pinda amewataka viongozi hao kudumisha amani katika dini zao, ilikuweza kuepuka vitendo viovu Vinavyo weza kuhatarisha amani.
Pinda amesisisitiza viongozi hao kuombea Jimbo la Kavuu ilikuweza kuepukana na magonjwa ya milipuko yanatokana na hali ya hewa.
Aidha amesema ni vyema kuweka ushirikiano baina ya serkali pamoja naviongozi wa dini kwani maendeleo yanatengemea pande zote mbili.
Wakizungumza viongozi wa dini katika kikao hicho wamesema changamoto kubwa wanazokutana nazo nipamoja na ukosefu wa Ardhi kwa ajili yakujengea makanisa na miskiti .
Pia wamesema kumekuwa na changamoto za Barabara kutokuwa kwa kiwango cha lami,maji, na umeme ambao umekuwa kero kwa kukatikatika ovyo na kukosekama kwa sehemu kubwa, uwepo makapuni yanayo ibia watu kwa kuchukua fedha zao kwa ajili ya nguzo na matokeo yake kuondoka bila kuwaingizia umeme .
Akijibu maswali ya viongozi hao amesema katika swala la maji pamoja na barabara ni swala ambalo mpaka sasa liko linafanyiwa kazi kwani maji yatatolewa katikakijji cha mamba mpaka sehemu zote za jimbo hili.
Pia amewashauri viongozi hao kuanza kulima mazao ambayo yanasoko la haraka kama vile Alizeti,Karanga na Ufuta ilikuweza kupata kipato cha haraka na chenye kukidhi mahitaji ya familia.
Sanjari na hayo amewataka viongozi kuzingatia kanuni za kiafya katika kupambana na virusi vya korona kwakuwahimiza waumini kunawa kwa Majitiririka ,Sabuni kuvaa Barakoa na kuepuka kukaa kwa kusogeleana wakati wakiwa Kanisani.
Hata hivyo viongozi hao wadini wamechagua kamati ya amani itakayo wawezesha kukutana na kujadili changamoto zao na kuwakilisha katika Serilkali ambapo viongozi wake Mwenyekiti ni Seifu Hassan,Makamu Mwenyekiti Vitusi Meza, Katibu Jems Haswaga,katibu msaidizi Simoni Kazumbagu ,Mhasibu ni Samson Mhondela.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa