Siku ya Kilele cha Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika Mkoa wa katavi yamefanyika kata ya Usevya katika Viwaja Vya Sharp RangersHalmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Leo tarehe 26 /4/2023.
Akizungumza na Wananchi Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi. Mwanamvua Hoza Mrindoko amesema zipo faida mbalimbali ambazo tumezipata kutokana na kuwepo kwa Muungano katika Mkoa wetu Hadi Nchi kwa ujumla amesema Kupatikana kwa Jina laTanzania Kumetokana na Muungano huu ambao umesababisha kuondoka kuitwa Tanganyika mpaka kuwa Tanzania.
Muungano huu umefanya kupatikana kwa Taifa moja lenye nguvu, kupatikana kwa mipaka Mipya baada ya Nchi hizi mbili, Kuwa na uchumi wa pamoja , uhuru wa Mtu kuishi popote , kupatikana kwa Uhuru wa kisiasa Baina ya pande zite mbili ,Hali ya ulinzi na usalama kuendelea kuimalika zaidi.
Serikali inayo ongozwa na Mhe.Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Miradi ya Elimu , Afya, Maji, Barabara, Umeme, Kilimo , ambapo Bilioni 620 zimetolewa kwa ajili ya Maendeleo .
Pia amewataka wananchi kuendelea kuwafundisha watoto Mila na Desturi nzuri za kitanzania ambazo hazina maadili potofu ambayo yatapelekea kupata tabia za Kishoga badala yake kuzalisha Taifa lenye vizazi Bora.
Maadhimsho ya Muungano yameenda Sambaba na kauli mbiu isemayo; Umoja na mshikamano ndiyo nguzo ya kukuza Uchumi wetu.
Mwisho
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa