Akizungumza na wananchi katika eneo la kata ya sitalike Halmashauri ya Nsimbo Wilaya ya Mpanda Mkoa Katavi katika Wiki ya MwanaKatavi ya Kilimo na Utalii Mkuu wa Mkoa Mhe.Mwanamvua Mrindoko amewataka wananchi kutunza Mazingira.
Akiwa katika wiki ya mwanakatavi ya kilimo na utalii amewataka wananchi kutumia vivutiao vilivilivyopo katika Mkoa wa Katavi Ilikuweza kiujionea uzuri wa maliasili ya zilizopo mkoani Hapo.
Amesema Mkoa wa Katavi ni Mkoa wa ambao umejaliwa kuwa na Hifadhi ya Katavi , vyanzo vya Maji , misitu ya asili , Uoto wa asili wa kuvutia na mito hivyo ni Nyema wananchi kuchukua jukumu la kulinda maliasili hizi zisiweze kuhalibiwa ilikuweza kukuza uchumi .
Aidha amewataka wanachi waache tabia kujihusisha na uwindaji haramu, kulima, kufunga na kuweka makazi katika maeneo ambayo siyo Rasmi, hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Katavi mwanamvua amawaongoza wananchi kutembelea hifadhi ya taifa ya Katavi ikiwa ni katika kuunga kitihada za Mhe. Samia Suluh Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ikumbukwe kuwa wiki ya Mwanakatavi ya kilimo na Utalii ilizunduliwa tarehe rasmi oktoba 28 2022. Ikiwa na lengo la kutangaza vivutio vya utalii
MWISHO.
Imeandaliwa na.
*Kitengo cha mawasiliano Serikalini.*
*Halmashuri ya Wilaya ya Mpimbwe*
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa