Wanawake wa Halamshauri ya wilaya ya Mpimbwe mapema leo Tarehe 1march 2023 wamefanya sherehe ya uzinduzi wa siku ya mwanamke katika kata ya Ikuba kijiji cha kashishi Mkoa wa Katavi.
wakiwa katika sherehe hiyo wamesema wanayofuraha kwa wiki hii maalum ambayo itawawezesha katika kujadili maswala mbalimbali yatakayo saidia kuinua maendeleo ya wanawake na kuepukana na maswala ya ukatili
Akizungumza mgeni rasm katika sherehe hiyo mhe Jenitha Sungura ambaye ni Diwani Vitimaalum Tarafa ya Mpimbwe amesema wanawake wanayonafasi kubwa katika famili kwani ndio walezi wakuu wa kuanzisha vizazi vyenye maadili na kuendeleza vizazi vitakavyokuwa nguzo imara katika Taifa kwa ujumla.
Aidha amewataka wanawake kuwapeleka watoto shule pasipo kujali njinsia ya watoto pia amesema mtoto wakike anayo nafasi ya kusoma kwani kumuozesha mtoto akiwa mdogo nikukosesha hakizake za Msingi.
Afisa Maendeleo ya jamii Daniely Saimon
amesema mwanamke anayo haki yakupewa thamani kama anavyopewa mwaname kwakuwa wote wanahaki sawa pia amewataka wanawake kuendelea kuepukana na masawala ya kuweka matabaka kwa watoto.
Ikumbukwe kuwa siku ya mwanamke Duniani kote Huadhimishwa March 8 ambapo lasimi huzinduliwa Tarehe 1 March na kusherekewa ndani ya siku saba ambapo wanawake hukutana na kujadili maswala mbalimbali .
Kaulimbiu ya Siku ya mwanamke inasema Ubunifu na mabadiliko ya teknologia chachu katika kuleta Usawa wa kijinsia.
Mwisho.
Imetolewa na
Ofisi ya mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa