Wataalam wa elimu ngazi ya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoa wa katavi wapatiwa mafunzo ya siku tatu ambayo yalianza Tarehe Februari 27, 2023 hadi Machi 01 katika ukumbi wa Shule ya msingi Majimoto
Mafunzo hayo yaliyohudhuriwa na washiriki 101 wakiwa ni Waratibu elimu kata , walimu wakuu wa shule za msingi 46, pamoja na wenyeviti wa kamati za shule .
Akifungua Mafunzo hayo Mratibu wa Shule Bora ngazi ya Halmashauri Bi Habiba Ngigwa amewataka washiriki kuendelea kuzingatia mafunzo wanayopewa kwa lengo la kuendelea kukuza elimu kwa kushirikiana na wazazi /jamii na walimu
Aidha amesema Ushirikiano wa Wazazi na Walimu (UWaWa )wanao wajibu wa kuhudhuria vikao shuleni, kusimamia usomaji wa wanafunzi nyumbani, kuibua na kuendeleza vipaji vya watoto, kuhamasisha uandikishaji wa watoto shuleni, mahudhurio pamoja na Mvuko wa wanafunzi kwenda sekondari, kuboresha miundombinu ya shule na kuimarisha mazingira salama na rafiki ya ujifunzaji ili kuchochea maendeleo ya taaluma shuleni
Pia amesema Mradi huu utasaidia kamati za shule katika maendeleo ya shule , kusimamia ustawi, kutatua changamoto za watoto wenye uhitaji Maalum pia kushushughulikia maswala ya ukatili .
Mafunzo hayo yameandaliwa na Mradi wa Shule Bora unaofadhiriwa na Serikali ya Uingereza kupitia mfuko wa UK aid kwa lengo la kuwajengea uwezo washiriki kwa ajili ya kuimarisha shughuli za UWaWa
Mwisho
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa