Halmashauri ya Mpimbwe tuna hatua nzuri ya ujenzi wa madarasa yatokanayo na fedha za uviko 19 zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Samia Suluhu Hassani .
Kauli hiyo imetolewa na timu za usimamizi na ufuatiliaji wa miradi wakati wa kikao cha kutoa tathimini ya hatua ya ujenzi wa madarasa yanayo jengwa kwa fedha za uviko 19 mbele ya mkuu wa wilaya ya Mlele Mh.Filberto Sanga
Baada ya kusoma maendeleo ya miradi kwa kila shule na kuonekana kufikia hatua nzuri wamesema juhudi pamoja na ushirikiano ndio chachu ya matokeo mazuri yanyoonekana kabla ya Tarehe inayo tarajiwa kuzinduliwa kwa majengo hayo kitaifa .
Kikao hicho kilicho wajumuisha madiwani walimu pamoja na wakuu wa idara mbalimbali kimeonyesha hali ya mwamko wakufanya kazi kwa bidii ukilinganisha na kipindi chanyuma ambapo mradi uliweza kuchukua mda mrefu bila kumalizika .
Akisoma taarifa kwa niamba ya mkurungenzi mtendaji, Mkuu wa idara ya mipango Anthony Danieli Kapula amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ilipokea fedha kwa ajili ya utekelezaji wa ujenzi wa vyumba 18 vya madarasa kwenye Shule Shikizi Msingi pamoja na sekondari ujenzi wa vyumba 31.
Baada ya mapokezi hayo Halmashauri iliweka mikakati mbalimbali ya kutekelza miradi ikiwa ni pamoja kuandaa mpango kazi, kuunda timu za usimamizi na ufuatiliaji na kusimamia zoezi la upatikanaji wa mafundi. Aidha, suala la manunuzi ya vifaa vya ujenzi pia liliweza kuratibiwa ili kupata vifaa pamoja kwa nia ya kufikia malengo kwa pamoja na kwa wakati.
Aidha fedha zilizopokelewa hadi sasa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii ni Tsh. 1,376,514,747.00
Naye Mkuu wa wilaya ya Mlele Mh. Filberto Sanga amesema amefurahishwa na hatua inayo endelea katika ujenzi kwani ujenzi umeendelea kwa kasi ya juu hali inayo tia moyo katika utendaji kazi .
Aidha amewataka timu za usimamizi kuhakikisha kunaandaliwa taarifa ya ununzi wa vifaa na pamoja na gharama zote zilizo tumika kutambulika ilikuweza kujua kiasi kilicho tumika na kilicho bakia kwa kila jengo .
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa