Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe imepokea Tsh. 1, 690,600,000.kupitia Mradi wa Boost kwa ajili ya Ujenzi wa Miundombinu mbalimbali Mradi huu utatekelezwa katika shule za Msingi, ujenzi wa vyumba vya Madarasa, Matundu ya Vyoo pamoja na shule mpya.
Halmashauri inatekeleza Ujenzi wa shule Mbili za msingi Mpya ambazo ni Kakuni na Maimba zitakazo gharimu Jumla ya Tsh 922,600,000.00 , Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 25 katika shule Saba za Bula 4, Kilida 4 , Makuyugu 3 , Mirumba 4 , Mkuyuni 4 , Nyambwe 4 na Migunga 2 yenye jumla ya Tsh 650,000,000.
Aidha Halmashauri inatekeleza Mradi wa ujenzi wa Matundu ya Vyoo 21 katika shule hizi ambapo ujenzi huo utagharim jumla yaTsh 46, 200,000 pia ujenzi wa Madarasa ya awali 2 katika shule ya msingi Ikuba yenye jumla ya 71,800,000.
Mradi huu unatekelezwa katika kata 6 ambazo ni kibaoni, Usevya Ikuba Majimoto Chamalendi na Mamba ambapo mpaka kufikia Tarehe 30 Jun mwaka huu Miradi yote itakuwa imekamilika .
Mwisho
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa