Wajumbe wa kamati ya siasa Mkoa wa Katavi wakiongozwa na mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa Ndugu Girbat Sampa wamefanya ukaguzi wa miradi ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi CCM 2020-2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe
Wakiwa katika Ziara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe wamekagua vyumba vitatu vya madarasa shule ya sekondari Usevya vilivyo jengwa kwa fedha za uviko 19 , Mabweni ya Wanafunzi shule ya Sekondari Usevya na kituo cha Afya Kibaoni .
Aidha Mjumbe wa kamati kuu Taifa Girbat Sampa amepongeza usimamizi wa miradi hii kwakuwa miradi imesimamiwa kikamilifu na kusisitiza kuzidi kusimamia kwa ukamilifu mradi wa ujenzi Kituo cha Afya cha kata ya Kibaoni na kuhakikisha kinakamilika pasipokuwa na mapungufu kwakuwa mpaka sasa hakuna makosa yoyote. .
Aidha Sampa amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa mambo mengi aliyoyafanya ndani ya mwaka mmoja ikiwa nipamoja na kuibua miradi mbalimbali ambayo inaonekana na kuleta tija kwa wananchi.
Nao wanachi katika kata ya kibaoni wameshukuru kupata kituo cha Afya kutokana na namna walivyokuwa wakipitia changamoto za huduma Ya Afya, ukosefu huo wa Kituo cha Afya ulikuwa ukisababisha wanawake wengi kuhangaika wakati wakujifungua.
Na Odetha Salumu
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa