Mkoa wa katavi umefanya maadhimisho ya siku ya Mtoto wa Afrika katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe katika viwanja vya shule ya Sekondari Mizengo Pinda Tarehe 16/06/2022.
Akizunguza Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mhe Mwanamvua Mrindoko amesema baadhi ya wazazi wamekuwa na tabia ya kuwafanyia ukatili Watoto kwanamna tofauti tofauti hivyo kuwakosesha haki zao za msingi.
Amesema baadhi ya wazazi wamekuwa wakiwatumikisha Watoto kazi ambazo hazistahili kwa umri wao na wengine kupewa ajira wakati wa muda wa masomo,kupewa kazi hatarishi kuwalawiti watoto wakiume na wakike kubakwa kutokana na mazingira wazazi kuwaamini waganga wa tiba za asili na kuwaachia Watoto kwa kwa lengo la kutibiwa usiku wakati mzazi hayupo badala yake wanafanyiwa matendo ya kikatili
Mkuu wa Mkoa Mhe Mwanamvua amesema wazazi wanatakiwa kijenga mazoea ya kuzungumza na Watoto ilikujua changamoto zinazo wakuta wawapo mbali nao kwani wazazi walio wengi hawaongei na Watoto badala yake wanakuwa wakali kwa watoto mpaka kufikia hatua ya mtoto kushindwa kujieleza kwa mzazi kwa kuhofia kupigwa au kufokewa.
akisoma taarifa kwa niaba ya Watoto Tabu Elbark Mwagonga Mwanafunzi wa Kidato cha kwanza shule ya sekondari Mizengo Pinda ameeleza chamgamoto wanazokutananazo watoto ikiwemo nikupigwa, kunyimwa chakula , kukosa Elimu, migogoro inayo sababisha wazazi kutengana , mila zisizo faa, watoto kupigwa , ubakaji , ulawiti, na Imani za kishirikina mambo yote hayo yanasababisha kumnyima haki zake mtoto.
ameiomba jamii ihamisishwe katika kumlimda mtoto na kukemea vitendo viovu dhidi yao.
Awali akisoma Taarifa Wilson Kenedy Afisa Maendeleo ya Jamii ambaye pia ni mratibu wa maendeleo ya mtoto Mkoa wa Katavi amesema Hali ya ukatili kwa Watoto katika Mkoa wa Katavi imepungua ikiwa katika kipindi cha mwaka 2020 hadi 2021 kwa Mkoa wa Katavi Mimba za utoto zilikuwa 1192, Ubakaji 59 utekelezaji wa familia 165 ndoa za utotoni 45 lakini kwa mwaka 2022 kuanzia mwezi Januari mpaka mwezi Juni mimba za utotoni ni 2, ubakaji 8 , utelekezaji familia 32, ulawiti 4, ndoa za utotoni 0 hali inayo onesha mabadiliko makubwa katika kupungua ukatili kwa mtoto.
Aidha ameishukuru serikali kwa kutoe elimu bila malipo kuanzia elimu ya msingi mpaka kidato cha sita pia ujenzi wa vyumba vya madarasa vitakavyowezesha Watoto kusoma katika mazingira mazuri na kupata elimu bora.
Kwa upande wake Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi ACP Ally Hamad Makame amesema jeshi la polisi katika mkoa wa Katavi lina endelea na kutoa Elimu kwa jamii ya kupinga ukatili wa kijinsia , kutokana na elimu hiyo jamii imejitahidi kutoa ushirikiano katika kukomesha vitendo vya ukatili.
ACP Ally Hamadi Makame amesema wazazi na walezi wanatakiwa kuendelea kutoa ushirikiano katika kuendeleza na kumlida mtoto dhidi ya vitendo vya ukatili.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa