Na odetha salum, Katavi.
Wanawake, Vijana ,na Walemavu Halmashauri ya Mpimbwe wamenufaika na mikopo inayotolewa na Halmashuri , kupitia mapato yake ya ndani inayowafanya wanawake kuweza kuinua uchumi wao kupitia kazi wanazozifanya .
Akizungumza Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii Godfrid Peter Nkuba ofisini kwake amesema kufikia mwezi wa Pili 2021 wameweza kukopesha vikundi 152, wanawake 90, Vijana 53 ,walemavu 9. Ambapo wametoa pesa takribani Milioni 540,500,000 Ambavyo imesaidia katika kuondokana na ukatili na unyanyasaji wa Kijinsia .
Amesema Idara yake imekuwa ikihamasisha Jamii katika kuibua miradi mbalimbali na kuitekeleza kwa kutumia Mikutano mbalimbali ya hadhara ili wananchi waweze kushiriki kuibua na kutumia nguvu zao katika kuiendeleza miradi hiyo .
Sanjari na hayo Nkuba amesema wameunda Kamati za ulinzi na Usalama zidi ya wanawake na Watoto ambazo zinasaidia kuondoa ukatili kufahamu wapi wanapaswa kupeleka madai yao pindi wanapo fanyiwa ukatili
Hata hivyo ameshauri wanavikundi kuharakisha kulipa mikopo yao kwa wakati ili kusababisha na wengine waze kupata fedha hizo, .
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa