• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara |
    • Anuani za watumishi |
Mpimbwe District Council
Mpimbwe District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Muundo wa Halmashauri
  • Utawala
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Fedha na Biashara
      • Mipango na Takwimu
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi na Mali asili
      • Kilimo , Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Kazi na zima Moto
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Mazingira na usafi
    • Kitengo
      • Ukaguzi wa ndani
      • sheria
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • ufugaji wa nyuki
      • TEHAMA na Habari
      • Ugavi na ununuzi
    • Sehemu
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Elimu
  • Machapisho
    • Muongozo
    • Hatua
    • Taarifa
    • Sheria
      • sheria ndogo
    • Fomu ya Maombi
      • Mkataba
    • Zabuni
  • Kituo cha Habari
    • Albamu ya Picha
    • Video
    • Mpya
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Matukio
    • Hotuba
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyopangwa

HALMASHAURI YA MPIMBWE YAHITIMISHA ZIARA YA MAFUNZO MBARALI

Posted on: June 21st, 2025

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe,  Mhe. Silas Ilumba,  Waheshimiwa Madiwani , na Mkurugenzi Mtendaji Bi. Shamim Mwariko, Timu ya Menejimenti na  Watumishi wafanya ziara ya mafunzo ya siku mbili kuanzia tarehe 18 hadi 19 Juni 2025 katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali, mkoani Mbeya. Lengo la ziara hiyo lilikuwa kujifunza kwa vitendo mbinu bora za kilimo cha kisasa cha zao la Mpunga, ukusanyaji wa mapato, pamoja na usimamizi wa rasilimali ndani ya halmashauri.

Katika ufunguzi wa ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mbarali, Bw. Stephene Katemba, aliwakaribisha rasmi wageni hao na kueleza kwa kifupi namna ratiba ya ziara hiyo itakavyokuwa. Pia, aliahidi kuwapatia ekari 15 kila mmoja kwa Mkurugenzi, Mwenyekiti pamoja na mtumishi mmoja wa Mpimbwe, ili waweze kujifunza kwa vitendo kilimo cha kisasa cha umwagiliaji.

Mafunzo ya kitaalamu kuhusu sekta ya kilimo yaliwasilishwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Mbarali, Bw. Yobu Mlomo, ambaye alieleza kuwa Halmashauri ya Mbarali ina vijiji 102 na kata 20, na imepiga hatua kubwa katika kilimo cha mpunga kutokana na matumizi ya mbegu bora aina ya SARO 5, mbolea za kisasa, na zana mbalimbali za kilimo.

Kwa mujibu wa Mlomo, uzalishaji wa mpunga umeongezeka kutoka gunia 7 hadi kufikia gunia 30 kwa ekari moja, huku baadhi ya wakulima wakivuna hadi gunia 43 kwa ekari. Katika msimu wa 2023/2024 pekee, tani 116.5 za mbegu bora za mpunga ziliweza kuzalishwa, na halmashauri iligharamia ukaguzi wa mashamba pamoja na kuwapatia wakulima mbegu.

Zaidi ya hapo, Halmashauri ya Mbarali inamiliki power tillers 5,987, matrekta makubwa 442, mashine za kupandia mpunga 29, mashine za kuvuna 146, mashine za kupura 78, za usindikaji 85, na maghala ya kuhifadhia 326. Wilayani humo kuna hekta 321,500 za ardhi ya kilimo, kati ya hizo hekta 98,567 zinafaa kwa umwagiliaji, pamoja na skimu 36 za umwagiliaji zilizoboreshwa na skimu 108 za asili.

Pia, wakulima 2,765 walifanyiwa upimaji wa afya ya udongo, na mashamba darasa 145 yaliundwa kwa ajili ya mafunzo ya kilimo shadidi (kilimo chenye matumizi kidogo ya maji na mbegu).

Mweka Hazina wa Mbarali Bw. Godson Mbelwa, alieleza namna halmashauri yao imefanikiwa kuongeza mapato kupitia ushuru wa mazao.

- Ushuru wa mchele:
  - 2021/2022: TZS 4,743,319,400
  - 2022/2023: TZS 3,295,727,400
  - 2023/2024: TZS 3,843,223,000
  - 2024/2025 (makadirio): TZS 4,417,816,000
- Ushuru wa mpunga 2021/2022: TZS 161,039,250

Mbinu walizotumia ni pamoja na: ushirikishwaji wa ofisi ya DC ,watendaji wa kata, , na doria usiku na mchana, uwepo wa vizuizi vya ukaguzi kila km 3–5, na urejeshaji wa 10% ya mapato kwa kata husika kwa matumizi ya POS na shughuli za ofisi za kata.

Katika siku ya pili ya ziara, ujumbe wa Mpimbwe ulitembelea Skimu ya Umwagiliaji ya Mbuyuni, Skimu ya Mto Mbarali, na mashine za uchakataji wa mpunga. Katika maeneo hayo walijionea kwa vitendo jinsi teknolojia ya kisasa inavyotumika kuongeza tija katika kilimo na usindikaji wa mpunga.

Kwa upande wa madereva na Afisa Usafirishaji wa Mpimbwe, walipata fursa ya kipekee ya kujifunza namna Halmashauri ya Mbarali inavyotengeneza magari yake yenyewe kwa ndani bila kuyasafirisha kwenda mbali, hali inayopunguza gharama za matengenezo kwa kiasi kikubwa.

Wakati wa kufunga ziara hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Mpimbwe Bi. Shamim Mwariko, alishukuru kwa mapokezi, ukarimu na elimu waliyoipata kutoka kwa wataalamu wa Mbarali. Alisisitiza kuwa mafunzo hayo ni muhimu kwa Mpimbwe na watahakikisha wanayafanyia kazi ili kuleta tija kwa wananchi.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mpimbwe, Mhe. Silas Ilumba, alieleza kuwa ziara hiyo imefungua mawazo mapya ya maendeleo, akiahidi kuhamasisha matumizi ya zana za kisasa za kilimo na kusimamia kwa karibu ukusanyaji wa mapato ndani ya Mpimbwe.

Matangazo

  • BOFYA HAPA KUONA ORODHA YA WANAFUNZI WALIOPANGWA KWENDA SHULE MOJA December 20, 2023
  • TANGAZO LA KAZI YA KUJITOLEA February 15, 2024
  • Tangazo la Nafasi za Kazi September 17, 2019
  • Tangazo la nafasi za Kazi za Muda April 21, 2020
  • Angalia yote

Habari Mpya

  • HALMASHAURI YA MPIMBWE YAHITIMISHA ZIARA YA MAFUNZO MBARALI

    June 21, 2025
  • MPANGO WA MATUMIZI YA ARDHI HALMASHAURI YA WILAYA YA MPIMBWE

    April 05, 2025
  • MKURUGENZI MTENDAJI WA H/W YA MPIMBWE AZINDUA MAFUNZO YA UWEZESHAJI WANAWAKE KIUCHUMI KWA WATENDAJI WA KATA NA VIJIJI

    February 12, 2025
  • BARAZA LA MADIWANI LA MPIMBWE LAWEKA MIKAKATI YA KUBORESHA LISHE NA MIRADI YA MAENDELEO

    February 11, 2025
  • Angalia yote

Video

Vivutio Vya Watali katika Hifadhi ya Taifa Katavi
Video Zaidi

Kiungo cha Haraka

  • Chuo kikiku cha kilimo Sua cha tembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe kwa ajili ya uanzishaji wa chuo cha kilimo Ndani ya Mkoa wa Katavi
  • Mpimbwe A Conservation and Development Project
  • Revenue collection dashboard for Katavi Region
  • Mkoa wa katavi

Kurasa za Karibu

  • NECTA
  • UTUMISHI
  • WIZARA YA ELIMU, SAYANSI, TEKNOLOJIA NA MAFUNZO YA UFUNDI
  • OR-TAMISEMI
  • Watumishi Portal
  • Tovuti ya ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Location Map

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya

    Sanduku la Posta: 245

    Telephone: 0625732265

    Mobile: 0625732265

    Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Maswali yanayoulizwa mara kwa mara
    • Ramani ya Mahali
    • Huduma

Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa