Akizungumza Afisa kilimo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Saadi Nyagawa akiwa katika mashamba ya wakulima wa mpunga, mahindi, karanga, na ufuta amesema Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ni Halmashauri ambayo wananchi wake wanategemea kilimo kutokana na Wananchi wa eneo hili hutegemea Zaidi Mvua ilikuweza kuzalisha Mazao mbalimbali.
Saadi Nyagawa amesema Halmashauri ya Mpimbwe inakadilia kulima kilimo cha mpunga Hekta 30 elf ambazo zitalimwa na kuzalisha Tani 120 kutokana na mvua kunyesha kwa wingi.
Aidha wakulima wako katika hatua mbalimbali za kilimo ikiwa katika zao la Mpunga tayari wengine wanapalilia na wengine wanapanda , lakina kwa zao la mahindi baadhi ya Mahindi yamechanua na mengine yakiwa katika hatua mbalimbali za ukuaji vivyo hivyo hata katika mazao mengine yakiwa katika hatua mbalimbali za ukuaji.
Kwa upande wake Mkulima Daniely Samsoni LYakajila amesema msimu wa Mwaka jana hakukuwa na mvua za kutosha hali iliyosababisha Kukosekana kwa Mazao mengi na kusababisha kupanda kwa bei yamazo hivyo kutokana na mvua kunyesha na utumia kulima mpunga kwa mistari anatarajia kuvuna gunia 40 kwa hekari.
MWISHO.
Imetolewa na
Kitengo cha mawasiliano serikalini
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa