Kupitia Baraza maalum la Hoja za Mkanguzi na Mthibiti wa hesabu za Serikali CAG Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Katavi BI. Jamilla Yusuph ameipongeza Halmashauri ya Wilaya Mpimbwe kwa kupata Hati safi kwa kipindi cha mwaka 2020/2021
Katika Baraza hilo Bi. Jamilla Yusuph amesema katika hoja hizo zilizofanyiwa ukaguzi na CAG kati ya hoja 60 ni hoja 28 tu ndiyo zilizopatiwa majibu ya kuridhisha na kufungwa na hivyo Hoja 32 sawa na asilimia 53 zimeendelea kusalia zikiwa katika hatua mbalalimbali za utekelezaji.
Bi. Jamilla ameitaka Halmashauri kuwachukulia hatua wale wote wanaosababisha kuendelea kuwepo kwa hoja kwa uzembe ikiwa hoja hizo zilikuwa ndani ya uwezo wao ili zisijirudie tena .
Pia amewataka Takukuru kufanya uchunguzi wa kiasi cha 137,858,361.60 ambazo ni nyongeza ya kazi katika mkataba wa ujenzi wa jengo la utawala bila ya mwajiri kujua kazi zilizoongezeka
Aidha amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh. Filbato Sanga kuhakikisha anasimamia Fedha zinazotolewa na Halmashauri kwa vijana , wanawake na watu wenye Ulemavu na Saccos kuhakikisha zinarejeshwa ili kuweza kusaidia na watu wengine .
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa