*15.11.2022*
*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Baraza la Madiwani la Halmshauri ya wilaya ya Urambo Mkoa wa Tabora wakiambatana na wakuu wa Idara kutoka halmashauri hiyo wamefanya ziara ya mafunzo ya kufuga na kuhifadhi nyuki.
Wakiambatana na Mwenyekiti wa Halmashuri ya Mpimbwe Sailas Irumba , Mkurungenzi mtendaji wa Halmashuri ya wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla, Waheshimiwa Madiwani wa Halmashauri ya Mpimbwe na baadhi ya Wakuu wa Idara, wametembelea katika chanzo cha chemichemi ya inayotoa maji yamoto kilichopo katika kijiji cha Majimoto ambacho hutoa maji yake ya moto ambayo ni asili, Pia wametembelea katika Chuo Kikuu cha Sokoine Tawi la Mizengo Pinda ambacho kipo katika Halmashuri ya Wilaya ya Mpimbwe kwa ajili ya kupata mafunzo ya ufugaji wa nyuki kwa kina .
Akitoa mafunzo ya namna ya kufuga nyuki pamoja na faida zake, Mhadhiri wa Chuo hicho Evaristus Magani amesema kuwa ufugaji wa kisasa unasaidia sana katika kuhakikisha upatikanaji wa asali na Nta unakuwa kwa wingi licha ya kuwa nyuki huzalisha mazao mengi ambayo watu hawajajua kuwa ni muhimu na hutokana na nyuki.
"Baadhi ya mazao kama Sumu ambayo huzalishwa kutokana na nyuki hufanya vizuri katika soko, chavua na mambo mengine ambayo hutokana na zao la nyuki." Amesema Magani.
"Ukataji wa miti umekuwa ukichangia kuondoa nyuki kutokana na kutokuwepo kwa maua hivyo ni muhimu kutunza mazingira hayo ili kukidhi mahitaji ya nyuki" Amesema Magani.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Urambo amesema wamefurahishwa kushuhudia maji katika mazingira hayo hasa kuona eneo lenye maji ya moto ambayo sehemu nyingine hawajabarikiwa kuyapata na ameshauri kukihifadhi chanzo hiki cha maji ambacho ni tunu kwa Halmashuri hii imepewa na Mungu, Pia amesema mafunzo waliyoyapata ya kufuga nyuki wangependa yawafikie wananchi wote ambao hujishungulisha na ufugaji wa nyuki katika Halmashuri ya Urambo.
Awali Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashuri ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla ametoa shukurani kubwa kwa Baraza hilo la Madiwa na Watumishi kutoka Urambo kuja kutembelea katika Halmashuri hiI kwa ajili ya kujifunza swala hilo, ni swala la kuigwa hata kwa wengine.
Bi. Mashalla amesema Halmashari hii inajishungulisha na kilimo zaidi na hata mapato yake ya ndani hutegemea zaidi kilimo hali ambayo huchangia katika uboreshaji wa miundo mbinu yake.
Naye mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe Sailas Irumba amewashukuru kwa kufika katika Halmashuri hiyo na kukubali kufika kuona chanzo cha maji ya moto na kuwaomba elimu waliyoipokea waifikishe kwa wananchi wao na Halmashauri wapo tayari kupokea wageni zaidi watakaofika kutembelea na kujifunza kuhusu ufugaji nyuki na kutembelea maeneo ya vivutio kama hayo.
Imetolewa na:
Kitengo Cha Mawasiliano Serikalini
*Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.*
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa