Ikiwa ni , tarehe 11 Februari, mwaka 2025 siku ya juma nne, Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe lilifanya kikao cha kawaida kilichohusisha madiwani wote pamoja na wakuu wa idara. Lengo kuu la kikao hiki kilikuwa ni kujadili njia bora za kutatua changamoto zinazokumba wananchi kwa ushirikiano wa pamoja.
Mwenyekiti wa kikao cha baraza, ambaye ni Diwani wa Kata ya Kasansa, Silas Ilumba, alifungua kikao kwa kusema kuwa suala la lishe linapaswa kuwa ajenda ya kudumu katika mikutano ya madiwani. Aliendelea kusema kwamba ni muhimu sana kuhamasisha jamii kuhusu kupanda miti ya matunda kama vile mapapai, machungwa, na nyinginezo, ili kupunguza tatizo la utapia mlo katika maeneo yetu. Alisisitiza kuwa, madiwani wanapaswa kuwa mabalozi wazuri katika kuhamasisha wananchi kupanda miti ya matunda kwa lengo la kuboresha lishe na kupunguza utapia mlo.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa