Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mkoani katavi Filbarto Sanga amewangoza watumishi wa Serikali za mitaa na viongozi wa Dini wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe katika zoezi la uzinduzi wa kuweka vibao vya Barabarani katika Tarafa ya Mamba na Tarafa ya Mpimbwe.
Katika uzinduzi huo, Sanga amewataka wananchi kuhakikisha wanatoa ushirikiano katika zoezi hilo ilikulifanikisha kama ilivyo pangwa.
Aidha amewataka wananchi kuendelea na kuweka vibao katika nyumba zao ilikuweza kurahisisha utoaji wa huduma ikiwa ni sambamba na kuendelea kulinda miundombinu ya vibao vinavyo wekwa katika barabara na mitaa.
Halmashauri ya mpimbwe imepokea Tsh milioni 70,767,291.69 kutoka serikali kuu kwa ajili ya kukamilisha zoezi hili .
Katika hatua nyingine, katika kikao na watumishi hao wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe DC Sanga amewataka watumishi kuhakikisha wanasimamia zoezi la Chanjo ya polio ilikila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano wahakikishe anapata chanjo hiyo .
Hata hivyo amewataka wananchi kutoa ushirikiano kwa watoa huduma watakao wakipita kutoa chanjo ilikuweza kufanikisha zoezi pasipo na usumbufu kwani kuto kufanya hivyo hatua kali za kisheria zitachukuliwa .
Na Odetha salum
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa