Mpimbwe ya zamani nitofauti na Mpimbwe iliyopo sasa kutokana na mabadiliko makubwa ya kimaendeleo yanayoendelea kuwepo tofauti na zamani .
Alexander Gabriel Maperani ni mzee anayeishi katika kijiji cha kibaoni kata ya kibaoni katika Halmshauri ya wilaya ya Mpimbwe anasema ukiangalia katika Sekta mbalimbali hali ilikuwa mbaya sana hasa katika nyanja za utawala , ulinzi ,Afya, Elimu, Miundombinu ya Barabara , Hali ya Mazingira na mila na Desturi .
Maperani amesema hayo mbele ya Mkuu wa Mkoa wa katavi Mwanamvua Mlindoko wakati wa kukabidhi Majengo ya Madarasa katika Shule ya Sekondari Mizengo Pinda
Ambapo amendelea kusema kulikuwa na changamioto kubwa sana katika hali ya usafiri hali iliyokuwa ngumu kutokana na Barabara kuwa mbovu ambapo msafiri ilikuwa inamgharimu wiki moja kusafiri kutoka Mpimbwe kwenda Mpanda hali iliyotofauti na sasa kwani kwa sasa msafiri anauwezo wakwenda na kurudi .
Amesema hapakuwa na shule za kutiosha Kwa ajili ya wanafunzi kusoma hali iliyokuwa ikiwalazimu kutumia umbali mrefu kwenda kupata Elimu japokuwa walio bahataka kuipata Elimu hiyo ni wachache ukulinganisha na wahitaji waliokuwepo jambo ambalo ni tofauti na sasa Shule zimejengwa kila mahali katika Halmashauri yetu ya Mpimbwe jambo ambalo ninzuri .
Sanjari na hayo hapakuwa na vituo vya kutolea Afya vingi kama ilivyo sasa kulikuwa na vituo viwili tu yaani Kituo cha Usevya na Mamba vilivyokuwa vikibeba Mzigo mkubwa kuwahudumia watu wengi tofauti na huduma iliyokuwa ikistahili kutolewa kwa kwa wakati .
Aidha amsema kutokana na viongozi kushirikisha wananchi mabadiliko yamekuwa kwa kasi kwani vikao vinafanafanyika na kushauriana nini kifanyike ilikuweza kuleta manufaa mazuri , licha ya ushirikishwaji wa wananchi lakini serikali inafuatilia nakujiua maendeleo ya kile kilichoanzishwa.
Pia katika swala la mila na desturi amewataka vijana kutowazarau wazee na kuona kama nisehemu ya kujivunia na kupata ushauri pale wanapotaka msaada wakimawazo lakini badala yake vijana wanasema “wamepitwa na wakati na wakati huo sisi tulikuwepo na sasa tupo na tunakokwenda tunakwenda pamoja “ amesema Mzee Maperani.
Hata hivyo amewataka wanafunzi kutumia muda wao vizuri wa masomo kwa kusoma kwa bidii na kuhakikisha wanapata nafasi nzuri katika masomo yao kwani Serikali imefanya jitihada kubwa kwa kupeleka Shule za sekondari pamoja na za msingi kila kona ya Tanzania .
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa