Na Odetha salum. Mpimbwe, Katavi
Beda Katani Mwenyekiti wa kamati ya siasa ya chama cha mapindunzi (ccm) mkoa wa Katavi amaefanya ziara ya kutembelea na kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Akiwa katika ziara hiyo iliyo ambatana na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Hawa Mlindoku ,na Naibu waziri wa sharia na katiba MH.Geofrey Pinda, Mh.Katani amekagua miradi ya ujenzi katika Shule ya Sekondari Mamba ,mradi wa ujenzi wa stendi ya Majimoto ,maghala manne ya kuhifadhia mazoa katika kijiji cha Mwamapuli ,utekelezaji wa ujenzi wa maji safi na salama katika Kijiji cha mwamapuli, mradi ujenzi wa wodi ya wazazi ,mradi wa ujenzi wa santation matundu ya vyoo vitano (5), chumba kimoja (1 )chakuongea wa mama wajawazito na usimikaji wa tenki la maji kibaoni .
Akitoa taarifa Mkurungenzi wa Halmashuri ya wila ya Mpimbwe Mh. Catherine Mashalla katika mradi wa ujenzi katika Shule ya Sekondari Mamba amesema Miradi inayotekelezwa kwa sasa katika shule ya sekondari ya Mamba ni Ujenzi wa Matundu 12 ya vyoo kwa chanzo cha fedha za COVID-19 (GPE), Ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasa kwa fedha ya Elimu lipa Kulingana na Matokeo (EP4R) na Ujenzi wa matundu 10 ya vyoo kwa fedha za Mfuko wa Jimbo.
Aidha amesema hadi sasa ujenzi wa Matundu 12 ya vyoo kwa chanzo cha fedha za COVID-19 (GPE) Mashimo ya vyoo yamekamilika, jengo la choo kimoja limepauliwa na lingine liko hatua ya Boma, ujenzi wa vyumba viwili (2) vya madarasaa na Ofisi kwa fedha za Elimu lipa kulingana na matokeo (EP4R) upo hatua ya uezekaji. Vyumba viwili vya Madarasa kwa fedha za Mapato ya ndani na Nguvu za Wananchi yako hatua ya upauaji. Ujenzi wa matundu 10 ya vyoo kwa fedha za Mfuko wa jimbo la Kavuu upo hatua ya ukamilishaji. Aidha kutakuwa na utengenezaji wa Madawati 80 kupitia fedha za lipa Kulingana na Matokeo ambapo kila Darasa ni Madawati 40.
Mkrungenzi mashalla amesema Ujenzi wa vyumba vya madarasa itasaidia kutatua changamoto ya msongamano wa wanafunzi katika vyumba vya madarasa na kutatua changamoto ya uhaba wa matundu bora ya vyoo,kuondoa maradhi ya mlipuko kama kipindupindu na maradhi ya matumbo kwa wana funzi .
Amesema shule hiyo aina kabiliwa na changamoto zifuatazo upungufu wa walimu wa sayansi 10 na Sanaa 5, upungufu wa matundu ya vyoo 15 ikiwa mahitaji ni 47 yaliyopo 32 upunngufu wa vyumba vya madarasa 7 ikiwa mahitaji
ni 22 yaliypo 15 hivyo ujenzi wa vyumba 4 utakapokamilika upungufu utakuwa vyumba 3.
Katika mradi wa ujenzi wa stendi ya majimoto amesema hadi sasa stendi ya Majimoto inaendelea kukua kwani kwa sasa kuna ongezeko la vyombo vya usafiri vinavyofanya safari zake ndani na nje ya Halmashauri. Pia, inapokea wasafiri kutoka nje ya Mkoa hivyo kufanya stendi ya Majimoto kukua zaidi na kufanya biashara kukua kwa kasi kulingana na mwingiliano wa watu,Uwepo wa stendi hii unasaidia kuongeza mapato ya Halmashauri kutokana na ulipaji wa ushuru kwa wawekezaji wa vibanda vya biashara na kodi kwa vyombo vya usafiri vinavyoingia na kutoka ambapo kwa mwaka mapato yanakadiriwa kiasi cha Tsh. 10,000,000.00.
Mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri ilipeleka kiasi cha Tshs. 10,000,000.00 kutoka na Mapato ya Ndani katika kijiji cha Migunga kwa ajili ya ujenzi wa vyoo bora katika Stendi ya Majimoto. Hadi sasa mradi uko hatua ya kuchimba mashimo na kupandisha Boma. Mradi huu utakapokamilika utasaidia kutatua changamoto ya ukosefu wa Vyoo bora hasa kuepusha mlipuko wa magonjwa kama vile kipindupindu na maradhi ya tumbo.
Mradi wa maghala ya mazao Mnamo mwaka 2010 Serikali ya kijiji cha Mwamapuli kwa kushirikiana na wananchi wa eneo la Mwamapuli kupitia mpango wa fursa na vikwazo (O&OD) waliibua mradi wa ujenzi wa maghala ya kuhifadhia mazao, Serikali ya kijiji ilitoa eneo lenye ukubwa wa ekari 65 kwa ajili ya mradi huu. Mradi huu unajumuisha uwepo wa maghala 4 ikiwa 3 ni kwa ajili ya kuhifadhi mazao na 1 limesimikwa mashine maalum kwa ajili ya kuongeza thamani zao la Mpunga.
Mradi huu ulianza kutekelezwa mwaka 2013 chini ya Halmashauri ya Wilaya ya Mlele kupitia Mpango wa Maendeleo ya Kilimo wa Wilaya (DADPs). Hadi kukamilika mradi huu uligharimu kiasi cha Tsh. 788,000,000.00, ikiwa Tsh. 738,000,000.00 ni ufadhili kupitia mpango wa DADPs na Programu ya MIVARF na Tsh. 50,000,000.00 ni michango ya nguvu za wananchi.
Aidha amesema changamoto kubwa ambayo imeikabili nikutokwepo kwa nishati ya umeme kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kusindika mazao kwa sababu mtambo huo unatumia Mafuta ya dizeli amabyo ni gharama kubwa kuuendesha
Hivyo Halimshauri imeomba kuwezeshwa transfoma kwa ajili ya kurahisisha uendeshaji wa Mtambo na suala hili linasimamiwa kwa karibu na Mhe: Mbunge Naibu Waziri wa Katiba na Sheria.
Katika Ujenzi wa mradi wa maji Kijiji cha Mwamapuli kinachopatikana katika Kata ya Mwamapuli Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ni miongoni mwa miradi inayotekelezwa kwa force account ambayo imedhaminiwa na mfuko wa PFR. Lengo la kuanzishwa kwa mradi huo ni kuhakikisha kuwa changamoto ya upatikanaji wa maji Safi na Salama katika Kijiji cha Mwamapuli Mradi huu ukikamilika utaweza kuhudumia Wananchi wapatao 4,193.
Mradi huu wa maji katika Kijiji cha Mwamapuli unagharimu kiasi cha tsh. 238,128,438.86 aidha mradi huu ulianza utekelezaji wake mnamo tarehe 20/6/2020 kwa maana ya hatua za manunuzi pamoja na maandalizi ya ujenzi na ulitarajia kukamilika tarehe 30/06/2021.Kiasi ambacho kimeshalipwa ni kiasi cha tsh 201,235,890.00.
Katika mradi wa wodi ya wazazi Mwaka 2020/2021 kiasi cha Tsh. 500,000,000.00 kilipokelewa kwa ajili ya ujenzi wa wodi 3 za watoto, Wanawake na wanaume. Wodi ya wanawake inakadiriwa kugharimu kiasi cha Tsh. 160,000,000.00 mpaka sasa utekelezaji wake upo hatua ya uezekaji. Ujenzi ulianza mwezi Aprili 2021 na unatarajiwa kukamilika mwezi Agosti 2021.
Hadi mradi huu utakapokamilika, utakuwa na uwezo wa kutoa huduma kwa wananchi wapatao 147,685 waliopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ikiwa ni pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili wananchi kama vile kupunguza vifo vya akina mama wajawazito pamoja na watoto chini ya umri wa miaka mitano na kuhudumia Wananchi waliokuwa wanapata matatizo makubwa ya kiafya na kwenda Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi ambayo ipo zaidi ya kilometa 125.
Mnamo mwezi wa sita 2020 kiasi cha Tsh. 24,000,000.00 kilipokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huu ambao una jumuisha ujenzi wa matundu 5 ya vyoo ikiwa matundu 4 ni kwa ajili ya wagonjwa wa kawaida, tundu 1 kwa ajili ya wenye mahitaji maalum, chumba 1 maalum kwa ajili ya kuogea wamama wajawazito na usimikaji wa tanki lita 5,000 kwa ajili ya kuhifadhia maji.
Kutokana na Mkataba mradi huu ulianza kutekelezwa Septemba, 2020 na ulitarajiwa kukamilika Desemba 2020. Aidha utekelezaji wake haukukamilika katika kipindi hicho kutokana na changamoto mbalimbali zilizojitokeza. Hadi sasa mradi huu umekamilika kwa kujenga miundombinu iliyokusudiwa.
Mradi huu wa ujenzi wa vyoo bora katika Zahanati ya Kibaoni umesaidia kutatua changamoto mbalimbali kama vile uhaba wa matundu bora ya vyoo hasa kupunguza msongamano wa wagonjwa, Wagonjwa wenye mahitaji maalum wameweza kupata huduma
Mh. Beda katani baada ya kutembelea miradi mbalimbali ameipongeza halmashauri pamoja na wananchi kwakujitoa katika kujenga miradi tofauti tofauti inayo endelea, pia katani ameshauri katika mradi wa ujenzi wa vyoo katika Shule ya Sekondari Mamba kuweka Maji kutokana na vyoo hivyo kujengwa bila kuwekwa mfumo wa maji.
Katika mradi wa mwamapuli kumekuwa na changamoto ya mradi kuwepo pasipo kufanya kazi jambo ambalo limeshangaza mwenyekiti wa kamati ya siasa kutokana na kutotolewa maelezo yenye kueleweka kwani mradi huo ni wawananchi na bado Halimashauri ilionekana kukondisha muwekezaji.
Nae Naibu Waziri wa Sheria na katiba geofrey pinda amepiga marufuku kwa Tarura kukataza Magari yanayobeba mizigo kukataliwa kufika katika maghala hayo kwa kusema barabara hizo hazipitishi Magari makubwa nijambo ambalo siyo sahihi na halitakiwi kwani wanachinchi wanatakiwa kupata huduma zote.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa