Wakiwa katika ziara hiyo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Wamekagua Miradi ya Ujenzi wa vyumba vya Madarasa Kupitia Mradi wa Boost yanayo endelea kujengwa katika shule za Bula , Makuyugu, Kilida ,Mirumba, Mkuyuni,Nyambwe, Ikuba, Kibaoni, Maimba, na Migunga Yenye Thamani ya Tsh 1,690,600,000.00.
Mwenyekiti wa Kamati ya Siasa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Mlele Mhe. Wolfugani Mizengopinda amewataka wasimamizi wa Miradi kusimamia kiukamilifu na kuzingatia Ubora wa viwango vya ujenzi vilivyo wekwa ili kuepuka kujenga Miradi isiyo na kiwango kinacho stahili ili kuweza kusaidia Miradi hiyo kukamilia kwa wakati na kusaidia kupunguza Msongamano wa wawanafunzi Darasani.
Joshua Mbwana ni Katibu wa CCM Wilaya ya Mlele Amemshukuru Dkt Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kujenga Miradi ya Maendeleo katika Jimbo la Katavi na Kavuu na kuendelea kuwajali watanzaia wote
Aidha Mbwana amesema wameridhishwa na ujenzi wa Miradi yote inayotekelezwa kwani inakwenda kwa kasi na kwa kuzingatia ubora.
Awali walitembelea Mradi wa Daraja la Mwamapuli ambalo nikiunganishi kikubwa kwa wanachi ambalo lilisababisha kuzorota kwa usafirishaji wa mazao
Pia walitembelea Shule ya Sekondari Mwamapuli kuangalia namna ambavyo Serikali inaendelea kutekeleza Miradi katika sehemu ambazo hazikuwa na shule.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa