Na, Odetha Salum, Mpimbwe, Katavi.
Akizungumza kamishina wa polisi Musa Ally Musa ( pichan) katika ukumbi wa shule ya Sekondari Usevya hapo jana uliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi, Afande Musa Ally Musa amesema mwaka 2006 Jeshi la polisi lilipata ushauri kutoka Vyuo Vikuu kutokana na matukio yaliyo kuwa yamekithiri kwa wakati ule, walipewa ushauri katika mambo matatu ya kuboresha ili kulifanya jeshi la polisi kuwa la kisasa kwakutumia technologia za kisasa, Weledi na kutumia mfumo unao husika na jamii yaani polisi jamii.
Kamishna wa polisi Musa Ally Musa amesema ilitolewa agizo kuwa kila kamanda wa polisi kuhakikisha anapeleka Polisi katika kila Kata na akae katika Kata pia Ofisi zake ziwe katika Kata ili aweze kuhudumia Jamii akiwa katika Kata hiyo.
Aidha amesema lengo la kupeleka Askari hao ni kuimalisha urinzi na usalama katika Kata, pia ili kutatu changamoto mbalimbali zinazo wakabili mwananchi ikiwa ni katika kero za maji, Watoto kuto kwenda shule mambo ya Mazingira na siyo kukamata wa halifu tu.
Pia amesema waligundua katika kata kuna kamati mbili mhimu ambazo zinafanya kazi kamati ya Maendeleo na kamati ya Ulinzi na Usalama ambapo Mwenyekiti wa kamati hizo ni Afisa Kata hivyo Jeshi la Poli likaona kuwepo kwa Polisi Kata ilikuweza kuwa katibu wa kamati ili kuweza kijadili changamoto ndani ya kata.
Hata hivyo amesema kumekuwa na changamoto za kutokuwepo kwa Askari kata katika kata jambo ambalo viongozi wa kata wakiwemo madiwani hawa ulizi kutaka kujua kwa nini hakuna polisi katika kata ilikuimarisha usalama wa wananchi na mali zao.
Kwaupande wake Kamishina mwandamizi wa polisi Afande Edibert Kyondo amesema katika matishio ambayo yana hatarisha hali ya kiusalama ni pamoja na Mazingira kwani katokana na Manzingira kuna migogoro mingi ambayo ipo katika Wafugaji na Wakulima pia migogoro ya Aridhi na maswala ya Misitu.
Pia amesema ili uweze kuimarisha hali ya Usalama lazima kuwepo na Polisi Kata ambaye anaweza kutembelea katika Shule mbalimbali kuwapa Elimu Watoto wa Kike ilikuweza kufahamu namna ya uepukana na vishawishi.
Hata hivyo amewataka kutengeneza program za mazingira ili kuweza kuepusha migongano ya kuhatarisha amani.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa