Wanawake kata ya Mwamapuli Halmashauri ya Mpimbwe Wilaya ya Mlele Mkoa wa katavi wamefanya sherehe ya Maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani leo tarehe 6 Mach 2023.
Sherehe hiyo ambayo kilele chake ni Tarehe 8 March ilianza kusherekewa rasmi tarehe 1 mwezi machi ambapo wanawake wanasherekea takribani wiki nzima.
Kaimu Mkurugenzi mtendaji Bi Toba Mwihanga ambaye ni Afisa Elimu, Elimu maalum amewataka wanawake kuwa vipaumbele katika kutetea watoto wakike na wakiume kwa kuwapeleka shule badala ya kuozeshwa na kupelekwa kuchunga mifugo " niseme tu kwamba sisi wanawake ndo wasemaji wa watoto wetu wewe mama ukinyamaza kusema hakuna atakaye mkomboa mwanao wanawake tuwapeleke watoto wetu shule anayestahili kuanza chekechea aanze pia kidato cha kwanza aanze kwa maana hao ndo Madaktari wa kesho msikatishe ndoto za watoto wapeni haki ya kusoma"
Aidha Diwani vitimaalum Mhe. Cellina Chacha akiwa katika sherehe hiyo amesema wanawake wamekuwabize nashughuli kuliko kufatilia maendeleo ya watoto kuanzia maisha ya nyumbani mpaka shuleni hali inayopelekea watoto wengi kuharibikiwa wakiwa na umri mdogo bila hata wazazi kujua.
" watoto wamekuwa wakifanyiwa ukatili wa aina nyingi ikiwemo kubakwa na kulawitiwa kutokana na wazazi kutokuwa makini na watoto halihizi ni mbaya na chafu"
Hivyo kila mwanamke achukue jukumu la lakuwa karibu na watoto kujua marafiki zake , kutambua aina ya michezo anayocheza mtoto akiwa na wenzake, na kutambua maendeleo yake ya shule .
Aidha amewataka wanawake kukaa na watoto wao wakike kuongea nao kuwaeleza halihalisi ya maisha pasipokuwaficha ili kuweza kuwasaidia kufikia ndoto zao.
Mwisho.
Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa