Kufatia ziara ya Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Majid Mwanga iliyo fanyika takribani wiki tatu kwa kutembelea na kukamilisha kata 9 ambazo ni Kibaoni, Usevya, Ikuba, Mwamapuli, Chamalendi, Mbende, Majimoto , Mamba, na Kasansa na kukamilisha vijiji vyote 31 vya Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Kutokana na Ziara hiyo iliyoibua changamoto mbalimbali zinazo wakabili wananchi ikiwemo suala la Chagulaga, matumizi mabaya ya Sungusungu, kutokusoma Mapato na matumizi kwa wananchi, upatikanaji wa Maji na Barabara kwa baadhi ya vijiji, na pamoja na migogoro ya Ardhi.
Mhe . Mkuu wa Wilaya amefanya Majumuisho ya Pamoja kwa njia ya Mjadala na watendaji wote wakiwemo Jeshi la polisi , Tarura, Ruwasa, Tanesco, Baraza la Ardhi, Watendaji wa Kata na Vijiji pamoja na Idara ya Elimu ngazi ya Kata na timu ya menejiment ya Halmashauri kwa kila mmoja kukumbushwa majukumu, vipaumbele , anayofanya katika eneo lake, na namna alivyo weza kushughulikia Kero zilizoibuliwqi wakati wa ziara.
Wakiwa katika Majumuisho hayo kila mmoja ameeleza namna ambavyo hutekeleza Majukumu yake.
Mkuu wa Wilaya amewataka kuendelea kufanya kazi kwa bidii, uaminifu na ubunifu ili kuweza kuwapa huduma Bora wananchi pia amewataka kufanya kazi kwa kutenda haki kwa Mtu yeyote unayemhudumia ilikuweza kuendela kutumikia Taifa kwa kikamilifu.
Baada ya kufanya mjadala huo viongozi hao wameshukuru kwa mjadala huo uliowafanya kila mmoja kujua na kukumbushwa namna gani anapaswa kufanya kazi na kutamani kuwa mijadala hiyo isiishie hapo badala yake iendelee.
Mjadala huo ulio ongozwa na Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Mpimbwe Bi. Shamim Mwariko kwa kuwa na mjadala mzuri kuanzia mwanzo hadi mwisho.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa