Wanawake katika Halmashauri ya Mpimbwe wameungana na wanawake wengine Duniani kote Kuazimisha siku ya wanawake duniani , maadhimisho hayo yamefanyika katika kijiji cha majimoto katika viwanja vya shule ya msingi majimoto .
Maadhimisho hayo yamefanyika leo tarehe 08 machi duniani kote ambapo wanawake katika halmshauri hii wametumia siku hii kuzungumza mafanikio , changamoto zao , ikiwemo msawala ya ukatili wa kijinsia ukosaji wa haki katika kumiliki Ardhi , na mambo mbalimbali. namna yakuzitatua changamoto Yanayo wakabili.
Wanawake wengi hupigwa , hubakwa , hupata mimba za utotoni , huuwawa , hukeketwa , na kukataliwa katika mambo ya urthi wa mali
Wanawake katika Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe wametumia siku hii kufundishana namna ya kuepuka na changamoto kwa kusema niwajibu wakila mwanamke kutimiza majukum yake kwa kutambua haki zake zamsingi na zakisheria ilikuweza kuepukana na changamoto zinazo wakabili, pia kutokuwa tegemezi bali kuchangamkia fulsa mbalimbali na kufanya shughuli za uzasiliamali , kilimo , kuchukua mkopa unao tolewa na Halmshauri ilikuweza kuutumia katika shughuli za uzalishaji mali na siyo kumtegemea mwanume peke yake.
. Akizungumza Catherine Mashalla Mkurungenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambaye ndiye mgeni rasmi katika maadhimisho haya amesema maswala ya usawa wa kijinsia yakianzia katika ngazi ya familia hakuna kutakacho pelekea wanawake kuonekana kutokuwa sawa na mwanaume katika Nyanja mbalimbali katika jamii .
Aidha ametumia nafasi hii kuwataka wanachi kutunza mazingira kwa kuepuka kuchoma misitu, kukata miti ovyo hali inayo hatalisha maisha kwa kusababisha ukosefu wa mvua za kutosha ,
Na Odetha Salum
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa