Kila mwaka ifikapo tarehe 8/3 Dunia inaadhimisha siku ya Mwanamke.Mkoa wa Katavi,Wilaya ya Mlele, Halmashauri ya Mpimbwe imeadhimisha Sherehe hiyo katika Kata ya Kibaoni leo tarehe 7/3, ikiwa ni kuelekea katika kilele cha siku ya Mwanamke.Kauli mbiu katika Maadhimisho hayo ni “Wekeza kwa Wanawake kuharakisha Maendeleo ya Taifa na Ustawi wa Jamii”,Katika Sherehe hiyo mgeni Rasmi alikua ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi.Shamim Mwariko .
Bi Shamim ameungana na Wanawake wote kutoka Halmashauri yetu ya Wilaya ya Mpimbwe kwa kupanda miti katika eneo lililopo kituo cha afya cha Kibaoni huku akiwakumbusha kutunza mazingira kwa kupanda miti, huku akiwakumbusha kuwa miti ni ishara ya Amani,Upendo, Mafanikio pia ni ishara ya Uhai. Anapokuwepo Mwanamke kunakuwa na uhakika wa kuongezeka Uhai ikiwemo Uhai wa Familia Uhai wa Kaya na Uhai wa maisha kwa Ujumla. Pia amewaomba kuendeleza upandaji wa miti ili kutunza mazingira.
Aidha Bi Shamim amewapongeza Wanawake juu ya ujasiriamari unaofanywa na Wanawake mbalimbali ili kujikwamua kiuchumi. Wanawake wametangaza Biashara zao mbalimbali zikiwemo ufumaji wa Mashuka, utengenezaji wa Maua, utengenezaji wa Viatu vya Ngozi, uchakataji wa Unga na kadharika.
Lakini pia mgeni rasmi ametoa Elimu kwa Wanawake namna ya kujikwamua kiuchumi kwa kujiunga katika Majukwaa ya ujasiriamali ambayo yanamuwezesha Mwanamke kujiongezea kipato na kutatua Changamato mbalimba za kimaisha na kuacha kuwa tegemezi.
Mwisho Bi Shamim amewaomba Wanaume kushirikiana na wanawake katika kujadili maswala ya kifamilia kwa Maslahi mapana kwa Familia na Taifa kwa ujumla na kuacha usiri wa kujimilikisha mali pasipo kumshirikisha Mwanamke,ameendelea kusema kuwa wanawake wapewe nafasi kwani sio vita bali ni katika kuikuza Jamii yenye tija.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa