Ushirikishwaji wa jamii katika kuibua Miradi mbalimbali ya Maendeleo umekuwa chachu ya kuifanya jamii kuwa sehemu ya miradi inayotekelezwa na Serikali katika nyanja tofauti tofauti , kupitia mfumo wa fursa na vikwazo kwa maendeleo ulio boreshwa O and OD utakao saidia kuimarisha ushiriki wa jamii katika kuibua Miradi sasa unakwenda kutekelezwa .
akifungua mafunzo kwa wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Mpimbwe katika ukumbi wa Halmashauri Mkurugenzi Mtendaji Bi. Catherine Mashalla amesema Mfumo huu wa O & OD Ni Mradi ulio kuwepo tangu awali ambapo umekuwa ukitekelezwa kwa wananchi Kwakuibua Miradi kwa kusaidiana na Serikali .
Amesema kupitia Mfumo huu ulio boreshwa wananchi wanapaswa kuibua Miradi mbalimbali ambayo wataikamilisha kuanzia mwanzo hadi mwisho .
Pia amewataka wakuu wa ldara kuonesha ushirikiano wakati wa utekelezaji wa Miradi ambayo wananchi wa taiibua ilikuweza kuondoa vikwazo vinanyo wakabili .
leonard tulubusya ambaye ni mwezeshaji naye amewataka Wakuu wa idara kuhakikisha wanawapa Wananchi elimu ya kutosha katika kushughulikia Swala la kuibua Miradi ilikuweza kujiongezea Fursa ambazo zitasaidia kuibua Miradi ya Kimaendeleo
amesema sambamba na kuwepo kwa mfumo huo hapo awali zipo changamoto zilizojitokeza wakati wa utekelezaji katika awamu nyingine zilizopo amesema hapo awali wananchi walikuwa wakitegemea ukamilishaji wa Miradi unategemea Serikali lakini kwa mfumo huu unahitaji wananchi kukamilisha miradi.
Godswine kodimbaya Mnufaika wa Mafunzo hayo ameipongeza Serikali kwa kupunguza vikwazo vinavyo jitokeza katika uibuaji na Utekelezaji wa Miradi ambayo utasaidia katika kuikwamua jamii.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa