TASAF awamu ya Tatu imelenga kuibua Miradi ya maendeleo itakayo toa ajira ya muda mfumpi kwa walengwa itakayo wasaidia kujiingizia kipato kupitia nguvu zao .
Akisoma taarifa mbele ya Mkurungenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi David Mziray mwakilishi wa Mkurungenzi TASAF amesema Miradi itakayo ibuliwa itafanywa na kaya zenye watu wenye uwezo wa kufanya kazi kuanzia umri wa miaka 18 hadi 65
David amesema Miradi hiyo inalenga kutoa ajira katika kipindi cha hali, ambapo walengwa itawasaidia wasishawishike kuuza rasilimali walizonazo kwa ajili ya kupata fedha , washiriki katika ujenzi wa miundombinu, waweze kupata kipato kitakacho wasaidia kuingiza ujira wa kaya na kupunguza umaskini
Nae Mkurungenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla Ameipongeza serikali kwa kuendelea kuboresha namna ambavyo itawasaidia wanufaika wa TASAF badala ya kupewa fedha kama ilivyo kuwa awali badala yake kufanya kazi zitakazo changia kukuza maendeleo .
Miradi hiyo itaibuliwa na wananchi kupitia mkutano wa kijiji utakao fanyika katika kijiji husika, ambapo watalaam wa Tasafu walio pata mafunzo ya namna ya kuibua miradi hiyo watasaidiana na walengwa kuhakikisha miradi hiyo inatekelezwa kwa ufasaha.
Na Odetha Salum
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa