Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe inatekeleza utoaji wa mikopo kwa makundi ya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ikwa ni dhamira ya serikali kuhakikisha kila Halmashauri inatoa mkopo wa 10% ya mapato yake ya ndani
Wanakikundi wa kikundi cha Nguvu ya Kazi katika kata ya Ikuba Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe walipokea Mkopo wa Tsh Million 15 kutoka katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe ambao umewawezesha kununua mashine ya kukoboa na kusanga Mahindi , kununua kiwanja kwa ajili ya ujenzi wa kituo chao cha kufanyia kazi na kuingiza umeme kwa ajili ya kuanza kusaga Nafaka .
Wakiwa katika uzinduzi huo wamesema wameishukuru Serikali kwa kuweza kuwainua vijana kwa kuwapa mkopo utakao wasaidia wao kujiajiri , wamesema mashine hiyo itasaidia kujiingizia kipato na kurahisisha huduma ya kusaga na kukoboa inapatikana kwa urahisi katika Kata ya Ikuba.
Godfrid Nkuba ni Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe akiwa ndiye Mgeni rasmi katika sherehe hiyo ya uzinduzi wa Mashine amesema Vijana wanapaswa kuiga mfano kwa Vijana wenzao nasiyo kuoneana wivu usio wa kimaendeleo amesema kikundi hiki wanapaswa kutumia vizuri kifaa hiki ili kuweza kupata manufaa makubwa kupitia mashine hii .
Pia amewaasa kuwa waangalifu wakati wanapokuwa wakitumia ili kisiweze kuharibika na kuwaletea matunda waliyokuwa wametegemea.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa