Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Comrade Juma Homera akitoa maelekezo baada ya kupokea na kujionea mradi wa ujenzi wa nyumba za wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe leo tarehe 27 Nov. 2020. Aidha Mh. Homera ameagiza mradi huo kukamilika ifikapo Dec. 31 2020 na wakuu wote wa Idara kuhamia iifikapo tarehe 0I Jan 2021.
Pia Mh. Homera ameitaka TANESCO kupeleka umeme katika mashine ya kupampu maji ndani ya siku 14 hadi 20 kuanzia leo 27.Nov.2020. Sambamba na hayo Mh.Homera amewapongeza watendaji wote wa Halmashauri kwa kazi nzuri ya usimamiaji wa miradi ya Halmashauri.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa