Mkuu wa Mkoa wa Katavi Mh.Mwanamvua H.Mrindoko alianza kwa kutoa elimu kuhusu umuhimu wa sensa kwa Nchi yetu na pia aliwaeleza wananchi umuhimu wa kutoa taarifa sahihi kwa Makarani kwani taarifa zote watakazotoa ni siri na zitatumiwa na serikali tu katika kuweka mipango ya maendeleo, kuweka mgawanyo sawa wa Rasilimali na huduma za Jamii kulingana na idadi ya watu wanaopatikana mahali fulani hivyo kila mtu anawajibu wa kutoa taarifa sahihi ili Serikali iweze kuwa na Takwimu sahihi za idadi ya watu,majengo na makundi maalum.
Sambamba na hilo pia alisema kwa mujibu wa sheria ya sensa namba 351 ya mwaka 2015 na marekebisho yake ya mwaka 2019 ni kosa kisheria kukataa au kugoma kutoa taarifa na kwa yeyote atakaye jaribu kufanya hivyo atachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria.
Mwisho Mh.Mrindoko aliwaomba wananchi wote kushiriki kikamilifu zoezi la sensa liatakofanyika kuanzia tarehe 23/08/2022 siku ya jumanne.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa