Mkurungenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe BI. Catherine Mashalla amekabidhi pikipiki 9 kwa Maafisa Ugani zilizo tolewa na Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania chini ya Wizara ya Kilimo , Umwagiliaji na Ushirika
Akikabidhi pikipiki hizo Catherine Mashalla Mkurungezi Mtendaji amesema pikipiki hizo zimetolewa na Serikali kwa lengo la kurahisisha usafili kumfikia Mkulima pindi anapohitajii ushauri wa kilimo
Amesema awali Maafisa Ugani walikuwa na chagamoto za kukosa usafili hali iliyokuwa ikipelekea Maafisa Ugani kuto wafikia wakulima kwa urahisi hivyo wakulima kuchelewa kupata ushauri wa kitalaam hivyo katika msimu ujao wakulima watanufaika na mazao yataongezeka .
Aidha amewataka kutumia pikipiki hizi kwa kazi iliyo kusudiwa na siyo kufanya shuguli ambazo hazijakusudiwa au kuzigeuza kuwa bodaboda
Awali akisoma Taarifa George Magile Afisa kilimo , umwagiliaji na ushirika amesema huduma za Ugani hutolewa kwa njia ya mashamba darasa ambapo kila afisa ugani huwa na shamba darasa moja kwaajiri ya wakulima kujifunza kwa nadhalia na vitendo .
Odetha kijika Afisa Ugani kijiji cha Usevya ameipongeza Serikali kwa Kwakutoa Pikipiki zitakazo wawezesha kufika kwa wakulima hali iliyokuwa ikiwapashida namna yakuwafikia wakulima katika maeneo ambayo haya fikiki kirahisi .
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa