Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko amemuagiza Katibu Tawala mkoa wa Katavi kufanya utambuzi wa madeni yote mapya na ya zamani ambayo Taasisi za Umma ndani ya mkoa huo zinadaiwa na wafanyabiashara ili waweze kulipwa fedha zao.
RC Mrindoko ametoa agizo hilo leo Mei 29, 2023 baada ya wafanyabiashara kuibua hoja ya mpango wa Serikali kuwalipa madeni yao, hoja iliyoibuka katika kikao cha kusikiliza kero za wafanyabiashara mkoani humo kilichoongozwa na Mkuu wa mkoa katika ukumbi wa madini wa Mpanda Social Hall uliopo mjini Mpanda.
Amesema kuelekea tarehe 26 Juni 2023 awe amepata ripoti ya madeni yote kutoka Ofisi ya mkoa na Taasisi zake, Ofisi za wilaya na Taasisi zake, Ofisi za Halmashauri na Taasisi zake ambazo wafanyabiashara wanadai.
Aidha, Mrindoko amesema mkoa umepokea takribani shilingi milioni 69 kutoka Serikali kuu kwa ajili ya kulipa madeni yote.
Hata hivyo, amewataka wafanyabiashara wote wanaoidai Taasisi yoyote ya Umma mkoani humo kujitokeza katika kikao atakachokifanya tarehe 26 mwezi Juni 2023 wakiwa na vielelezo ili kumaliza mkanganyiko uliopo wa baadhi yao kutolipwa madeni yao muda mrefu.
Katika hatua nyingine, RC Mrindoko amewaagiza viongozi wote kuanzia ngazi ya juu hadi ngazi ya mtaa kuwa waadikllifu na kuyaheshimu makundi yote ya wafanyabiashara wala kusiwepo bughudha za aina yoyote kwani ni watu muhimu katika kulijenga Taifa.
Pia amewataka mamlaka ya Mapato (TRA) mkoa wa Katavi kuwa waaminifu kwa wafanyabiashara ikiwemo kutumia busara wakati wa kukusanya kodi badala ya kumpa vitisho na kumfungia biashara yake.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa