Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh. Filbarto Sanga amefanya kikao na Watendaji wa Kata Watendaji wa Vijiji, Wenyeviti wa vijiji, Walimu Wakuu wa shule ,na wakuu wa Idara mbalimbali katika ukumbia wa shule ya Msingi Majimoto katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi 13/10./2022.
Akiwa katika kikao hicho cha kuandaa mpango mkakati wa ujenzi wa Madarasa amesema Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan ametoa kiasi cha shalingi Milioni 460 kwa ajili ya Ujenzi wa Vyumba vya Madarasa 23 ambavyo kila Darasa moja lita gharimu kiasi cha shililingi Milion 20 ikiwa ni maandalizi ya Wanafunzi wa kidato cha kwanza kwa mwaka 2023.
Mh Filbarto amesema Miradi inayoletwa na Serikali kuu nivyema ikasimamiwa kiukamilifu ili kuweza kukamilika kwa wakati kwakuwa Madarasa hayo yatasaidia kuondoa changamoto wa upungufu wa Madarasa katika halmashauri ya Mpimbwe.
Licha ya kuondoa changamoto ya upungufu Madarasa lakini Halmashauri ya Wilaya ya Mpimwe inakabiliwa na chamgamoto ya Watoto kutembea umbali mrefu kufika shuleni swala amabalo tayari lilikuwa limekwisha anza kufanyia ufumbuzi kwa kuanzisha ujenga shule ya Sekondari Kabunde ambapo tayari Wananchi wamekwisha kuanza kuweka nguvu kazi na shule ya Sekondari Ikulwe inayojengwa katika kata ya majimoto.
Kutoka na fedha hizo zilizotelewa na Serikali Mh. Filbarto Sanga ameonya vikali baadhi ya watumishi kuomba kiasi cha fedha kwa Mkandarasi au fundi anayepewa jukumu la kujenga Madarasa kabla ya kupewa kazi jambo amabalo linasababisha fundi kushindwa kuwalipa wasaidizi wake kutokana na fundi kubaki na kiasi ambacho hakikidhi kuwalipa Nafundi wasaidizi.
Hivyo amewataka kuacha mara moja kwakuwa niswala ambalo lina tia aibu na kuiaibisha Halmashauri.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa