Afisa Maendeleo ya Jamii Finias Nderwa akitoa elimu kwa wanakikundi wa Kata ya Kasansa na kata ya Majimoto Juu ya Matumizi bora ya uhifadhi wa mazingira kwa kufuga Nyuki kwa ajili ya kuwaletea maendeleo yao.
Akiwa katika kata hizo amesema Mradi huu amabao unakwenda kuwanufaisha wanakikundi tayari umeshaanza kutekelezwa kwa kutengeneza mizinga ambayo kwa kila kikundi ambacho wanatarajia Kufunga Nyuki watapewa Mizinga 52 ambapo mizinga hiyo itaambatana na vifaa vyote ambavyo husaidia katika hatua zote za uvunaji wa nyuki.
Aidha amewataka wanakikundi hawa kuendelea kuwa tayari katika kuhakikisha wanapata manufaa katika Mradi huu wa urejeshwaji wa Mazingira
Mwisho.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa