Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mh. Filbato Sanga amegawa vitabu kwa wadau wa Elimu na kutoa maelekezo kwa wadau katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Mkoani Katavi.
Akiwa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Usevya amesema vitabu hivyo vya aina tatu vitasaidia katika kuboresha elimu nakuweka misingi bora ya kuimarisha kiwango cha elimu katika nchi ,vitabu hivyo ambavyo ni Mwongozo wa uteuzi Viongozi Elimu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa na Mikao ,Mkakati wa kuimarisha Ufundishaji na ujifunzaji ngazi ya Elimumsingi, na Changamoto katika uboreshaji Elimu Msingi na Sekondari(Nini kifanyike)
Amesama awali hapakuwa na mwongozo wa namna ya kuwateua walimu Wakuu wa shule hali iliyokuwa ikipelekea kuwepo kwa changamoto za namna wanavyo weza kuongoza ikiwa walimu wakuu walikuwa wakiteuliwa pasipo kuwa na utaratibu wowote
Mh.Mkuu wa Wilaya amesema kupita miongozo hiyo itasaidia mamlaka zinazohusika katika kuteua walimu wakuu wa shule kusimamia miongozo ambayo itaonesha sifa za kiongozi husika anayestahili kuongoza katika shule husika kwa shule ya msingi na sekondari, .
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe Bi. Catherine Mashalla amesema Watoto wetu watapata Elimu inayohitajika hivyo niwajibu wakila mdau kusimamia miongozo hiyo ambayo imetolewa na serikali .
Baadhi ya wadau wa elimu katika Halmashauri ya Mpimbwe wameishukuru serikali kwa kutoa miongozo itakayosaidia kuteu viongozi mbalimbali pia miongozo hiyo itasaidia kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kutokana na walimu kufundisha kwa kufuata miongozo jambo litakalo epusha baadhi ya shule kufaulu na Shule nyingine kufeli.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa