Mapema leo tarehe 27.12.2022 Mkuu wa Wilaya ya Mlele Mhe. Filbarto Sanga amezindua utoaji wa huduma ya Tiba Kituo cha Afya Majimoto kilichopo ndani ya halmashauri ya Mpimbwe kata ya Majimoto Kijiji cha Ikulwe Mkoa wa Katavi.
Kuzinduliwa kwa utoaji wa huduma ya Tiba kituoni hapo kumekuja kufuatia utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa alilotoa tarehe 14/12/2022 baada ya jengo la wangongwa wa nje kukamilika ipasavyo kituoni hapo.
Agizo hilo limetekelezwa na Mhe. Filbarto Sanga mara baada ya kukamilisha maagizo ambayo Waziri Mkuu ambapo alihitaji yatekelezwe na kituo kuanza kufanya kazi, aidha katika ziara yake Waziri Mkuu Majaliwa alimuagiza Mkurungenzi wa halmashauri hiyo kuhakikisha vifaa vyote vinavyo hitajika vifike kwa wakati na wananchi kuanza kupata matibabu katika kituo hiki.
Akizindua utoaji wa huduma ya Tiba kituoni hapo Mhe. Sanga amesema kituo hicho kimejengwa kwa kutumia mapato yake ya ndani ya Halmashauri hiyo ambapo kiasi cha shilingi Milioni 423,890,000.00 zimetumika kukamilisha ujenzi huo ambapo kitanufaisha wakazi wapatao 31,842.
Kwa mjibu wa mkataba wa ujenzi huo, ujenzi ulianza mnamo tarehe 19.01.2021 na ulitarajiwa kukamilika 20.02.2023 ambapo ulihusisha ujenzi wa jengo la wagonjwa wanje, jengo la mama na mtoto, jengo la upasuaji, jengo la maabara, jengo la kufulia na ujenzi wa vyoo matundu 7 kituoni hapo.
"Tumezindua utoaji wa huduma ya Tiba katika kituo chetu cha Afya hapa kata ya Majimoto rasmi leo, ni matarajio yetu wananchi wote wa kata hii na maeneo jirani watanufaika na huduma bora zitakazo patikana hapa ikiwa ni za awali na za msingi lengo likiwa ni kuwapunguzia adha wananchi ya kutembea umbali mrefu kuitafuta huduma kama itakayo tolewa hapa" amesema Mhe. Sanga.
Katika hatua nyingine, Mhe. Sanga amewataka wataalamu wa Afya waliopelekwa kufanya kazi kituoni hapo, kuzingatia misingi ya taaluma zao wakati wakutoa huduma kwa kutoa kauli nzuri kwa wangonjwa na kuhudumia pasipo kuwa na ubaguzi wa aina yoyote kwa wananchi wote.
Naye diwani wa kata ya Majimoto Grace Udoba ameishukuru serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuwasogezea wananchi huduma ya kituo cha Afya ambayo itasaidia kupuguza ubali mrefu waliokuwa wakiutumia wananchi wa eneo hilo wakupata huduma hiyo.
Kwa upande wake Bi. Neema Majola mkazi wa kata ya Majimoto kwaniaba ya wananchi wa eneo hilo waliohudhuria uzinduzi wa utoaji wa huduma ya Tiba katika kituo hicho cha Afya amemshukuru Mama Samia Suluhu Hassan kwa kuwakumbuka wana majimoto kwani kuletwa kwa kituo hicho kitawasaidia wanawake wajawazito kuepukana na vifo wakati wakujifungua na pia watapata matibabu wakati wote na kwa urahisi.
Imetolewa na.
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini.
Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa