Wananchi Mkoani Katavi wametakiwa kutumia fursa ya maonyesho ya Wiki ya Mwanakatavi kujifunza masuala mbalimbali ya Kilimo na Utalii ili kunufaika na fursa mbalimbali zilizopo katika Sekta hizo Ili kujikwamua Kiuchumi.
Rai hiyo imtolewa na Mkuu wa Wilaya ya Mlele Bw.Filberto Sanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi Bi.Mwanamvua Hoza Mrindoko katika uzinduzi wa maonyesho ya Kilimo na Utalii ikiwa ni maadhimisho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii iliyofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Kashato Manispaa ya Mpanda
Bw.Sanga amewahimiza Wananchi kutumia vyema manyesho hayo kujifunza fursa mbalimbali katika Sekta ya Kilimo na Utalii zinazopatikana ndani ya Mkoa wa Katavi jambo litakalosaidia kuimarisha uchumi wa Mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.
Aidha Bw.Sanga ametoa rai kwa Taasisi za Uhifadhi wa Maliasili Mkoani Katavi kuelekeza nguvu ya ziada katika ulinzi wa Maliasili hizo ikiwemo Misitu na Wanyamapori ili kunusuru rasilimali hizo dhidi ya Wavamizi.
Amewataka Maafisa Ugani Mkoani Katavi kuhakikisha wanawasajili wakulima wote kwa kuwa lengo la zoezi hilo licha ya kufanikisha zoezi la uuzaji wa mbolea ya ruzuku pia linalenga kutambua idadi ya Wakulima wote Nchini
.Katika hatua nyingine Bw.Sanga amelitaka shirika la kuhudumia Viwanda Vidogo Nchini SIDO kujenga uwezo kwa Wajasiriamali juu ya namna ya kukuza mitaji yao ili kujikwamua na Umasikini.
Awali Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Katavi Bw.Nehemia James katika ufunguzi wa Maonyesho ya Wiki ya Mwanakatavi ya Kilimo na Utalii amesema lengo la maonyesho hayo ni kutoa fursa kwa Wananchi Mkoani humo kujifunza masuala mbalimbali kuhusu Kilimo na Utalii pamoja na kubaini fursa zilizopo katika Sekta hizo.
MWAISHO.
*Imeandaliwa na*
kitengo cha mawasiliano Serikalini.
*Halmashauri ya Wilaya ya Mpimbwe.*
Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe- Usevya
Sanduku la Posta: 245
Telephone: 0625732265
Mobile: 0625732265
Barua Pepe: ded@mpimbwedc.go.tz
Haki miliki @2017 Halmashauri ya wilaya ya Mpimbwe. Haki zote zimehifadhiwa